Hadithi za Maandiko
Katika Umoja wa Imani—Yesu Kristo analiongoza Kanisa Lake kupitia mitume na manabii


Waefeso 2:19–20; 4:11–14

Katika Umoja wa Imani

Yesu Kristo analiongoza Kanisa Lake kupitia mitume na manabii.

Paulo na Mitume wengine wakiwabatiza na kuwathibitisha waumini wapya wa Kanisa.

Mitume wa Yesu waliihubiri injili Yake katika nchi nyingi. Watu walioiamini injili walibatizwa. Mtume Paulo alitaka kila mtu ajisikie kukaribishwa katika Kanisa la Mwokozi, hata kama walikuwa wanatoka sehemu tofauti tofauti.

Mathayo 28:19–20; Waefeso 2:19

Yesu akiwa na watu waliokusanyika kumzunguka.

Paulo aliandika barua kwa Watakatifu katika Efeso. Alisema kwamba Yesu alipokufa kwa ajili yetu, ilikuwa ni kama Yeye alivunja ukuta ambao uliwatenganisha watoto wa Mungu. Bila kujali chimbuko lao, hawakuwa wageni tena. Wangeweza kuipokea injili na kuwa sehemu ya “nyumba ya Mungu,” kama familia moja kubwa!

Waefeso 2:11–19

Yesu akifundisha kundi la watoto, kukiwa na jiwe la pembeni la jengo kwa mbele.

Paulo alisema kwamba Kanisa ni kama jengo imara. Majengo yanahitaji msingi imara. Jiwe muhimu zaidi katika msingi ni jiwe kuu la pembeni. Mawe mengine yote yanapangwa kufuata jiwe la pembeni. Yesu Kristo ni jiwe kuu la pembeni la Kanisa Lake.

Waefeso 2:20

Picha za watu wakifundisha, wakihudumu, na kushiriki injili.

Sehemu iliyobakia ya msingi wa Kanisa ni manabii na mitume, ambao wanamshuhudia Yesu Kristo. Bwana pia anatualika sote kusaidia kulijenga Kanisa Lake—kwa kufundisha, kwa kuhudumu, kwa kushiriki injili, na katika njia zingine nyingi.

Waefeso 2:20; 4:11–12

Kundi la watoto wakija pamoja katika umoja.

Kanisa linahitajika, Paulo alisema, ili kumsaidia kila mtu kumjua Yesu Kristo. Kanisa la Yesu Kristo lipo duniani leo, likiwa na msingi imara wa Yesu Kristo na manabii na mitume Wake. Kupitia Kanisa Lake, tunaweza kukua “katika umoja wa imani” na kuwa zaidi kama Yesu.

Waefeso 2:21–22; 4:13