Hadithi za Maandiko
Njoo Uone—Kumwalika rafiki kumfuata Yesu


Yohana 1:43–51

Njoo Uone

Kumwalika rafiki kumfuata Yesu

Filipo akimsikiliza Yesu anapowafundisha watu.

Mtu aliyeitwa Filipo alikuwa mmoja wa wafuasi wa Yesu. Alijua kwamba Yesu alikuwa Mwokozi. Filipo alitaka Nathanaeli rafiki yake ajue pia kuhusu Yesu.

Yohana 1:43–45

Filipo akizungumza na Nathanaeli rafiki yake.

Nathanaeli alijua kwamba maandiko yalisema Mungu angemtuma Mwokozi. Filipo alimwambia kwamba alikuwa amempata Mwokozi—jina Lake lilikuwa Yesu, kutoka Nazareti.

Yohana 1:45

Filipo akimwalika Nathanaeli kuja na kumwona Yesu.

Mwanzoni Nathanaeli hakumwamini. Hakufikiria kwamba Mwokozi angeweza kuwa wa kutoka Nazareti. “Laweza neno jema kutoka Nazareti?” aliuliza. Filipo alijibu, “Njoo uone.”

Yohana 1:46

Yesu akimsalimu Nathanaeli.

Nathanaeli alienda na Filipo kukutana na Yesu. Wakati Yesu alipowaona wakija, Yeye alisema kwamba Nathanaeli alikuwa mtu mwema na mwaminifu. Nathanaeli alishangaa. Hakuwahi kukutana na Yesu hapo awali. Ni kwa jinsi gani Yesu alimjua?

Yohana 1:47–48

Yesu akizungumza na Nathanaeli.

Yesu alimwambia Nathanaeli kwamba kabla ya Filipo kuzungumza naye, Yesu alikuwa amemwona amekaa chini ya mti wa mtini.

Yohana 1:48

Nathanaeli akipiga magoti kwa Yesu.

Sasa Nathanaeli aliamini kwamba Yesu alikuwa Mwana wa Mungu. Yesu alimwambia Nathanaeli angeona mambo makubwa—kama malaika wakitoka mbinguni—yote kwa sababu ya imani yake.

Yohana 1:49–51