Mathayo 14:22–33
Kutembea juu ya Maji
Imani hushinda hofu
Yesu alitaka muda wa kuwa peke yake ili kusali. Yeye aliwatuma wanafunzi Wake katika mashua upande mwingine wa Bahari ya Galilaya. Yesu alienda kusali mlimani.
Mathayo 14:22–23
Usiku ule, upepo ulikuwa mkali, na mawimbi yalikuwa makubwa. Wanafunzi wa Yesu walifanya kazi kwa bidii usiku mzima wakijaribu kuifikisha mashua upande mwingine wa bahari.
Mathayo 14:24–25
Usiku ulipokaribia kuisha, wanafunzi walimwona mtu akitembea juu ya maji kuwaelekea. Walidhani kilikuwa ni kivuli, na waliogopa. Hakikuwa kivuli; alikuwa ni Yesu! Yeye aliwaita, akasema, “Jipeni moyo; ni mimi; msiogope.”
Mathayo 14:25–27
Petro alimwomba Yesu amwalike aje Kwake juu ya maji. Yesu alisema, “Njoo!” Petro alitoka nje ya mashua na kuanza kutembea juu ya maji, kama vile Yesu!
Mathayo 14:28–29
Lakini Wakati Petro alipoona upepo mkali na mawimbi makubwa, aliogopa. Alianza kuzama ndani ya maji. Alimwita Yesu, “Bwana, niokoe.”
Mathayo 14:30
Yesu alimfikia na kumshika Petro. Yeye alimuuliza Petro kwa nini alitilia shaka badala ya kumwamini Yeye zaidi.
Mathayo 14:31
Wakati Yesu na Petro waliporudi kwenye mashua, dhoruba ilikoma. Wanafunzi walishangazwa na kile kilichotokea. Walijua kwamba Yesu alikuwa kweli Mwana wa Mungu, na walimsujudia.
Mathayo 14:32–33