Hadithi za Maandiko
"Mmenitendea Mimi"—Tunapowatumikia wengine, tunamtumikia Yesu


Mathayo 25:31–46

"Mmenitendea Mimi"

Tunapowatumikia wengine, tunamtumikia Yesu

Yesu akirudi duniani.

Yesu Kristo aliwaambia wanafunzi Wake kwamba baada ya Yeye kurudi kwa Baba Yake wa Mbinguni, Yeye atarudi duniani pamoja na malaika wote watakatifu. Siku hiyo, watu kutoka mataifa yote watakusanyika mbele Yake—watu ambao walimfuata Yeye na watu ambao hawakumfuata.

Mathayo 25:31–33

Mtu akimpa chakula mtu mwingine.

Yesu atawaambia watu waliomfuata wangeweza kuingia katika ufalme Wake, kwa sababu alipokuwa na njaa, walimlisha. Yeye alipokuwa na kiu, walimpa Yeye kinywaji.

Mathayo 25:34–35

Msichana akimtembelea mwanamke mwingine ambaye ni mgonjwa.

Walimpa Yeye nguo na mahali pa kukaa wakati Yeye alipohitaji. Yeye alipokuwa mgonjwa au gerezani, walimtembelea.

Mathayo 25:36

Yesu akifundisha kuhusu jinsi ya kupendana na kumpenda Yeye.

Watu watamwuliza Yesu wakati ni gani walifanya chochote kati ya vitu hivi vya ukarimu kwa ajili Yake. Mwokozi ataelezea kwamba tunapofanya mambo ya ukarimu kwa watu wengine, ni kama tunafanya mambo mazuri kwa niaba Yake.

Mathayo 25:37–40

Mwanamke anakataa kuwapa chakula watu wenye shida.

Yesu atasema kwa watu ambao hawakumfuata Yeye kwamba hawawezi kuingia ufalme Wake. Yeye alipokuwa na njaa na kiu, hawakumpa Yeye chakula au kinywaji.

Mathayo 25:41–42

Mtu mwenye shida amekaa peke yake.

Hawakumsaidia wakati Yeye alipohitaji nguo au mahali pa kukaa. Yeye alipokuwa mgonjwa au gerezani, hawakumtembelea.

Mathayo 25:43

Yesu anaendelea kufundisha kuhusu jinsi ya kupendana na kumpenda Yeye.

Yesu ataelezea kwamba tunapochagua kutomsaidia mtu mwenye shida, tunachagua kutomsaidia Yeye. Tunapochagua kuwasaidia wengine, tunachagua kumsaidia Yesu.

Mathayo 25:45