Hadithi za Maandiko
Yesu Anawafariji Wanafunzi Wawili—Matembezi ya pamoja njiani kuelekea Emau


Luka 24:13–43

Yesu Anawafariji Wanafunzi Wawili

Matembezi ya pamoja njiani kuelekea Emau

Wawili kati ya wanafunzi wa Yesu wakitembea kuelekea Emau.

Siku ambayo Yesu alifufuka, wanafunzi wawili walikuwa wakitembea kutoka Yerusalemu hadi mji uitwao Emau. Walikuwa wafuasi wa Yesu, na walikuwa na huzuni. Walikuwa wakizungumza wao kwa wao kuhusu kifo cha Yesu na vitu vingine ambavyo vilitokea katika siku chache zilizopita.

Luka 24:13–14

Yesu anatokea na anatembea pamoja na wanafunzi hawa. Wanafunzi hawatambui kwamba ni Yesu.

Walipokuwa wakitembea, Yesu alikuja na kutembea pamoja nao, lakini hawakujua ilikuwa ni Yesu. Yeye aliuliza kile walichokuwa wakikizungumzia na kwa nini walikuwa na huzuni.

Luka 24:15–17

Wanafunzi wanaelezea kwamba Yesu alikuwa amekufa.

Walishangaa Yeye hakujua kilichokuwa kimetokea. Walimwambia Yeye kuhusu Yesu. Walifikiri Yeye angekuwa Mwokozi wao, lakini Yeye alikuwa amekufa.

Luka 24:18–21

Wanafunzi wanasema kwamba mwili wa Yesu umetoweka kutoka kaburini.

Pia walisema kwamba baadhi ya wanawake walikuwa kaburini Mwake, lakini mwili wa Yesu ulikuwa umetoweka. Malaika walikuwa wamewaambia wanawake kwamba Yesu alikuwa hai.

Luka 24:21–24

Yesu anawafundisha wanafunzi.

Yesu kisha akawafundisha kile maandiko yalisema kuhusu Mwokozi. Yeye alisema manabii walikuwa wamefundisha kwamba Mwokozi angekufa na kufufuka tena.

Luka 24:25–27

Yesu anabariki mkate na kuwapa wanafunzi.

Walipofika Emau, ilikuwa usiku sana. Wanafunzi hao wawili walimwalika Yesu kukaa pamoja nao. Yesu aliketi chini kula pamoja nao. Yeye alitwaa mkate, akaubariki, na kuwapa wanafunzi. Wakati huo, walijua alikuwa ni Yesu. Ghafla Yeye alitoweka.

Luka 24:29–31

Wanafunzi wanazungumza kuhusu uzoefu wao na Yesu.

Wanafunzi hao wawili walizungumza kuhusu jinsi walivyojisikia vizuri mioyoni mwao wakati Yesu alipokuwa akiwafundisha kutoka kwenye maandiko. Waliharakisha kurudi Yerusalemu kuwaambia wanafunzi wengine kwamba walikuwa wamemwona Yesu.

Luka 24:32–35