Hadithi za Maandiko
Malaika Anamwachilia Huru Petro kutoka Gerezani—Mungu anajibu sala


Matendo ya Mitume 12:1–17

Malaika Anamwachilia Huru Petro kutoka Gerezani

Mungu anajibu sala

Petro akiwekwa gerezani.

Mfalme aliyeitwa Herodi hakuwapenda Wakristo. Alimuua Mtume Yakobo. Kisha akamweka Petro gerezani. Aliwaweka askari 16 kulinda gereza.

Matendo ya Mitume 12:1–4

Watu wakisali kwa ajili ya Petro.

Waumini wa Kanisa waliposikia haya, walisali na kusali kwa Baba wa Mbinguni kwa ajili ya Petro.

Matendo ya Mitume 12:5

Petro akiwa amelala gerezani.

Usiku mmoja, Petro alikuwa amelala. Alikuwa amefungwa na minyororo miwili katikati ya askari wawili.

Matendo ya Mitume 12:6

Malaika akimtokea Petro.

Ghafla, nuru ikang’ara gerezani, na malaika akatokea. “Inuka upesi,” malaika alisema, na minyororo ikaanguka kutoka mikononi mwa Petro. Malaika alimwambia Petro amfuate.

Matendo ya Mitume 12:7–8

Malaika akimwongoza Petro kuwapita walinzi.

Petro alidhani alikuwa anaota ndoto. Alimfuata malaika akiwapita walinzi. Lango la chuma ambalo liliongoza kwenda mjini lilifunguka lenyewe, na Petro na malaika wakapita.

Matendo ya Mitume 12:9–10

Petro anatembea peke yake mjini.

Malaika aliondoka, na Petro aligundua hakuwa anaota ndoto. Alijua Bwana alikuwa amemtuma malaika kumwokoa.

Matendo ya Mitume 12:10–11

Petro anagonga mlango wa nyumba ya Mariamu.

Petro alikwenda nyumbani kwa mwanamke aliyeitwa Mariamu, mahali ambapo waumini wengi wa Kanisa walikuwa wamekutana humo kusali. Alibisha hodi mlangoni.

Matendo ya Mitume 12:12–13

Roda anasikia sauti ya Petro nyuma ya mlango.

Msichana aliyeitwa Roda alikuja mlangoni. Aliposikia sauti ya Petro, alifurahi sana! Alikimbia kwenda kuwaambia wengine.

Matendo ya Mitume 12:13–14

Roda akiwaambia waumini wa Kanisa kwamba Petro yupo mlangoni.

Wakati Roda alipomwambia kila mtu kwamba Petro alikuwa mlangoni, hawakumwamini. Petro aliendelea kubisha hodi.

Matendo ya Mitume 12:15–16

Petro anawaambia waumini wa Kanisa kwamba Bwana alimtoa gerezani.

Hatimaye, walifungua mlango na kuona kwamba ilikuwa ni kweli. Petro alikuwa salama! Bwana alikuwa amejibu sala zao. Petro alimwambia kila mtu jinsi Bwana alivyomtoa gerezani.

Matendo ya Mitume 12:16–17