1 Wakorintho 15
Katika Kristo Wote Watahuishwa
Paulo anafundisha kuhusu ufufuo
Baadhi ya waumini wa Kanisa katika mji unaoitwa Korintho walikuwa na maswali kuhusu kile kinachotokea baada ya kufa kwetu. Hawakuwa na uhakika kwamba Yesu kweli alikuwa amefufuka. Baadhi ya watu walisema kwamba hakukuwa na ufufuo tena. Paulo alisikia kuhusu hili na kuandika barua kwa Watakatifu huko Korintho.
1 Wakorintho 15:12–14
Paulo aliandika kwamba Ufufuko wa Yesu Kristo ulikuwa sehemu muhimu ya injili Yake. “Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu,” Paulo alisema, na “akafufuka tena siku ya tatu.” Zaidi ya watu 500 walimwona baada ya Ufufuko Wake, akiwemo Paulo na Mitume wengine.
1 Wakorintho 15:1–8
Paulo alifundisha kwamba kama Kristo asingefufuka, sisi sote tungekuwa na huzuni na bila tumaini. Kwa sababu ya Anguko la Adamu, sisi sote tutakufa, lakini kwa sababu ya Yesu Kristo, sisi sote tutafufuka pia!
1 Wakorintho 15:17–22
Paulo aliwakumbusha Watakatifu huko Korintho kwamba watu walikuwa wakibatizwa kwa niaba ya wafu. Kwa nini tungehitaji kufanya hivyo kama watu waliokufa kamwe hawangefufuliwa tena? Tunabatizwa kwa niaba ya wafu kwa sababu tunajua kila mtu ataishi tena. Hii inawapa nafasi ya kupokea baraka za Bwana.
1 Wakorintho 15:29
Baadhi ya Watakatifu huko Korintho walijiuliza miili yetu itakuwaje wakati tutakapofufuka. Paulo alisema miili yetu itakuwa mitukufu. Haitakuwa miili dhaifu au kupata magonjwa au kuzeeka. Baadhi ya watu watakuwa na miili ya selestia, inayong’aa kama jua. Wengine watakuwa na mng’aro kama mwezi, na wengine watakuwa na mng’aro kama wa nyota.
1 Wakorintho 15:35, 40–43; Mafundisho na Maagano 76:96–98; 88:20–23