Hadithi za Maandiko
Yesu Anamponya Mwanamke na Kumfufua Binti wa Yairo—”Usiogope, amini tu”


Marko 5:21–43

Yesu Anamponya Mwanamke na Kumfufua Binti wa Yairo

“Usiogope, amini tu”

Yairo pamoja na mke wake na binti yake.

Mtu aliyeitwa Yairo aliishi na mke wake na binti yake katika mji karibu na Bahari ya Galilaya. Yairo alikuwa kiongozi katika sinagogi, ambapo Wayahudi walienda kumwabudu Mungu.

Marko 5:22

Binti wa Yairo anaumwa sana.

Binti wa Yairo, ambaye alikuwa na umri wa miaka 12 tu, aliumwa sana. Alikuwa karibu kufa. Yairo alijua alihitaji msaada. Pia alijua kwamba Yesu alikuwa katika mji wao.

Marko 5:22–23

Yairo anamwomba Yesu amponye binti yake.

Yairo aliondoka nyumbani kwake na kumtafuta Yesu. Alipiga magoti miguuni pa Yesu na kumwomba Yeye aje kumponya binti yake. Yairo alijua kwamba kama Yesu angembariki binti yake, angeishi. Yesu alimfuata Yairo nyumbani kwake. Umati wa watu ulimfuata Yesu.

Marko 5:23–24

Mwanamke katika umati anataka kuponywa na Yesu.

Mwanamke katika mji huo pia alihitaji msaada wa Yesu. Alikuwa mgonjwa sana kwa miaka 12. Alikuwa ametumia pesa zake zote kwa madaktari, lakini hakuna ambaye angemponya—aliendelea kuwa na hali mbaya. Alijua kwamba Yesu angeweza kumponya. Lakini ni kwa jinsi gani angemfikia Yeye kupitia umati ule?

Marko 5:25–27

Jesus Heals Woman Raises Jairus' Daughter

Mwanamke huyu aliamini kwamba kama yeye angegusa tu mavazi ya Yesu, angeweza kuponywa. Alimfikia Yesu alipokuwa akitembea. Mara tu alipogusa pindo la vazi Lake, ugonjwa wake uliponywa.

Mathayo 9:20; Marko 5:27–29; Luka 8:44

Yesu anauliza ni nani aliyemgusa.

Mara moja, Yesu aliacha kutembea. Alikuwa amehisi nguvu zimemtoka. “Nani aliyenigusa?” Aliwauliza. Wanafunzi wake walikanganyikiwa. Watu wengi walikuwa wamemgusa Yeye—walikuwa wamezungukwa na watu. Yesu alitazama kote ili kuona ni nani aliyemgusa.

Marko 5:30–32; Luka 8:45

Yesu anamwambia yule mwanamke aende kwa amani.

Yesu alimwona mwanamke aliyegusa mavazi Yake. Alimwambia Yesu kuhusu ugonjwa wake, na kwamba Yesu alikuwa amemponya. Yesu alimwambia afarijiwe. Aliponywa kwa sababu ya imani yake Kwake. “Nenda kwa amani,” Yeye alimwambia.

Marko 5:33–34; Luka 8:47–48

Yairo anapata habari kwamba binti yake amefariki.

Kisha mtu akatoka katika nyumba ya Yairo. Alisema kwamba walikuwa wamechelewa sana: Binti wa Yairo alikuwa tayari amefariki. Yairo hakupaswa tena kumsumbua Yesu.

Marko 5:35.

Yesu anamwambia Yairo amwamini Yeye.

Mara Yesu aliposikia haya, Yeye alimwambia Yairo, “Usiogope, amini tu.” Kisha wakaenda nyumbani kwa Yairo.

Marko 5:36–38

Yesu anamwambia binti wa Yairo ainuke.

Yairo na mke wake walimwongoza Yesu hadi pale binti yao alipolala. Yesu aliushika mkono wa msichana na kumwambia, “Inuka.”

Marko 5:41

Binti wa Yairo yu hai tena.

Mara moja, binti wa Yairo aliamka kutoka kitandani mwake. Hakuwa mfu tena! Yesu aliwaomba Yairo na mke wake wamletee kitu cha kula. Walishangazwa na kile Yesu alichokifanya kwa ajili ya binti yao. Yeye aliwaomba wasiwaambie watu wengine kuhusu muujiza huu.

Marko 5:42–43