Mathayo 20:1–16
Mfano wa Wafanyakazi katika Shamba la Mizabibu
Ujumbe wa matumaini
Yesu aliwaambia wanafunzi Wake mfano au hadithi ili kuwasaidia kuelewa ufalme wa mbinguni ukoje. Katika mfano huo, mtu alihitaji watu kufanya kazi katika shamba lake la mizabibu. Kwa hiyo, mapema asubuhi moja, aliwapata baadhi ya wafanyakazi waliokubali kufanya kazi siku nzima kwa sarafu moja. Walianza kufanya kazi.
Mathayo 20:1–2
Saa tatu baadaye, mtu huyo aliajiri wafanyakazi zaidi. Aliwaomba wafanye kazi katika shamba lake la mizabibu kwa siku nzima. Aliahidi kuwalipa vizuri.
Mathayo 20:3–4
Saa tatu baada ya hapo, mtu huyo alipata hata watu wengi zaidi waliohitaji kazi. Aliwaomba wafanye kazi katika shamba lake la mizabibu pia.
Mathayo 20:5
Hatimaye, karibu na mwisho wa siku, mtu yule aliwaona watu ambao hawakuwa na cho chote cha kufanya. Walisema hakuna mtu aliyewapa kazi yo yote siku nzima. Mtu huyo alisema wanaweza kufanya kazi saa ya mwisho ya siku katika shamba lake la mizabibu.
Mathayo 20:6–7
Mwisho wa siku ya kazi, mtu yule anawalipa wafanyakazi. Alitoa sarafu moja kwa watu ambao walikuwa wamefanya kazi kwa saa moja. Pia alitoa sarafu moja kwa kila mmoja wa wafanyakazi wengine. Watu waliofanya kazi siku nzima walikasirika. Walidhani wanapaswa kupata pesa zaidi kuliko kila mtu mwingine.
Mathayo 20:8–12
Mtu huyo aliwakumbusha wafanyakazi hao kwamba walikuwa wamekubaliana kufanya kazi siku nzima kwa sarafu moja. Alisema hawapaswi kukasirika kama alichagua kuwa mkarimu kwa wengine ambao walifanya kazi katika shamba lake la mizabibu.
Mathayo 20:13–16