Hadithi za Maandiko
Yesu Anawaomba Mitume Kuwalisha Kondoo Wake—Kuonyesha upendo kwa Yesu kwa kuwafundisha wengine kumhusu Yeye


Yohana 21; Mathayo 28:16–20; Marko 16:15–19

Yesu Anawaomba Mitume Kuwalisha Kondoo Wake

Kuonyesha upendo kwa Yesu kwa kuwafundisha wengine kumhusu Yeye

Petro na Mitume wengine wanaenda kuvua samaki.

Baada ya Yesu kufufuka, Petro na baadhi ya Mitume wengine walienda kuvua samaki. Japokuwa walivua samaki usiku mzima, hawakuvua chochote.

Yohana 21:1–3

Yesu anawauliza Mitume kama wamevua samaki wowote.

Asubuhi iliyofuata, Mitume walimwona Yesu ufukweni, lakini hawakujua ni Yeye. Yeye aliuliza kama walikuwa wamepata samaki wowote. Walisema hawakuwa wamepata.

Yohana 21:4–5

Mitume wakijaribu kuvuta nyavu iliyojaa samaki ndani ya mashua.

Yesu aliwaambia Mitume watupe nyavu zao upande wa kulia wa merikebu na wangevua samaki. Mitume walifanya kile Yesu alichosema, na zaidi ya mia moja samaki walijaza wavu! Wavu ulikuwa mzito sana na samaki kiasi kwamba Mitume hawakuweza kuivuta ndani ya mashua.

Yohana 21:6

Petro anaogelea kumwelekea Yesu.

Kisha Yohana akatambua mtu yule alikuwa nani. Alimwambia Petro, "Ni Bwana." Petro aliruka ndani ya bahari na kuogelea kumwelekea Yesu. Mitume wengine walileta mashua na samaki ufukweni. Yesu alikuwa akipika mkate na samaki, na Yeye aliwaalika Mitume kula pamoja Naye.

Yohana 21:7–13

Yesu anamwambia Petro awalishe wanakondoo Wake.

Baada ya kula, Yesu alimwuliza Petro, "Je, wanipenda kuliko hawa?" Petro alisema ndiyo. Kisha Yesu akasema, "Lisha kondoo zangu."

Yohana 21:15

Petro anamwambia Yesu kwamba anampenda Yeye.

Kisha Yesu akamwuliza Petro tena kama alimpenda Yeye. Tena, Petro akasema ndiyo. Yesu alimwambia, "Lisha kondoo wangu."

Yohana 21:16

Yesu anamfundisha Petro kuwatunza watu wanaomfuata Yeye.

Yesu alimwuliza Petro mara ya tatu kama alimpenda. Petro alisema, "Bwana, wewe wajua yote; wewe umetambua ya kuwa nakupenda." Yesu alimwambia tena, "Lisha kondoo wangu." Yeye alitaka Petro awatunze watu wanaomfuata Yesu.

Yohana 21:17

Yesu anawaambia Mitume kushiriki injili.

Baadaye, Yesu aliwaomba Mitume Wake kukutana Naye mlimani. Hapo Yeye aliwaambia washiriki injili Yake ulimwenguni kote, wafundishe watu amri Zake, na wabatize kila mtu aliyeamini. "Nanyi mtakuwa mashahidi wangu," Yeye alisema. Yeye aliahidi angekuwa pamoja nao na kuwapa nguvu kupitia Roho Mtakatifu.

Mathayo 28:16–20; Marko 16:15–19; Matendo ya Mitume 1:8

Yesu anapaa mbinguni.

Kisha Yesu akaenda juu angani katika wingu. Yeye alirudi kwa Baba Yake wa Mbinguni. Mitume walipomtazama akiondoka, malaika wawili walitokea. Walisema kwamba kama vile Yesu alivyokuwa amekwenda mbinguni, Yeye atarudi duniani kwa njia hiyi hiyo siku moja.

Matendo ya Mitume 1:9–11