Hadithi za Maandiko
Karamu ya Mwisho—Yesu anaanzisha sakramenti


Mathayo 26; Luka 22; Yohana 13–14

Karamu ya Mwisho

Yesu anaanzisha sakramenti

Yesu na Mitume Wake katika Yerusalemu.

Yesu na Mitume Wake walikuwa Yerusalemu kusherehekea Pasaka. Wayahudi walisherehekea Pasaka kila mwaka. Iliwasaidia kukumbuka kwamba, miaka mingi iliyopita, familia zao zilikuwa watumwa huko Misri, na Mungu aliwasaidia kutoroka.

Kutoka 12:27

Yesu na Mitume Wake walikusanyika kuzunguka meza.

Walipokuwa Yerusalemu, Yesu na Mitume Wake walikuwa na karamu maalum pamoja. Yesu alikuwa akitazamia kushiriki chakula hiki pamoja nao.

Luka 22:7–15

Yesu akiosha mguu wa mmoja wa Mitume Wake.

Baada ya kumaliza kula, Yesu alijaza bakuli kwa maji. Yeye alianza kuosha miguu ya Mitume Wake.

Yohana 13:4–5

Petro akiuliza kwa nini Yesu anaosha miguu yao.

Ilipofika zamu ya Petro, aliuliza kwa nini Yesu alikuwa anafanya hivi. Kuosha miguu ilikuwa kitu ambacho kwa kawaida watumishi tu ndio walifanya.

Yohana 13:6

Yesu akiwafundisha Mitume Wake kuhusu jinsi ya kupendana.

Yesu alisema alikuwa akiosha miguu yao ili kuwaonyesha wao mfano. Yeye aliwataka kutumikiana na kupendana kama Yeye alivyowapenda. Kama wangefanya hivi, watu wangejua walikuwa wanafunzi Wake.

Yohana 13:14–16, 34–35

Petro akizungumza na Yesu.

Yesu aliwaambia wanafunzi Wake kwamba Yeye angekufa hivi karibuni. Petro alisema alikuwa tayari kufa kwa ajili ya Yesu.

Yohana 13:36–38

Yesu akimjibu Petro.

Lakini Yesu alijua nyakati ngumu zilikuwa zinakuja. Yeye alimwambia Petro kwamba kabla ya jogoo kuwika asubuhi iliyofuata, Petro angesema mara tatu kwamba Yeye hakumjua Yesu.

Yohana 13:38

Yesu akiwafundisha Mitume Wake kuhusu Roho Mtakatifu.

Yesu alijua kwamba Mitume Wake wangeweza kuwa na wasiwasi na kuogopa. Yeye aliahidi kwamba Mungu angewatumia wao Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu angewafariji, kuwafundisha, na kuwasaidia kukumbuka kile Yesu alichowafundisha. Yeye aliwaambia wasiwe na wasiwasi au kuogopa. Yeye alisema, "Mkinipenda, mtazishika amri zangu."

Yohana 14:1, 15–16, 26–27

Yesu akimega mkate kwa ajili ya sakramenti.

Kisha Yesu alifanya kitu maalumu sana kuwasaidia Mitume Wake daima kumkumbuka Yeye. Yeye aliwapa wao sakramenti. Kwanza, Yeye alibariki mkate, akaumega vipande vipande, na kuwapa Mitume Wake. Yesu aliwaambia wafikirie juu ya mwili Wake wakati walipokula mkate ule. Yeye aliwaomba wakumbuke kwamba Yeye angekufa kwa ajili yao.

Mathayo 26:26; Luka 22:19

Yesu akibariki divai kwa ajili ya sakramenti.

Yesu kisha akamimina divai kwenye kikombe. Yeye alibariki divai na kuwaambia Mitume wainywe. Yesu aliwaambia wafikirie juu ya damu Yake wakati walipokunywa divai. Yeye aliwaomba wakumbuke kwamba Yeye angeteseka, kutokwa na damu, na kufa kwa ajili ya maumivu na dhambi za watu wote ili tuweze kutubu na kusamehewa.

Mathayo 26:27–28; Luka 22:20

Yesu akiwafundisha Mitume Wake kutii amri Zake.

Kisha Yesu akaelezea kwamba Yeye ni kama mzabibu, na wanafunzi Wake ni kama matawi. Kama tawi litabaki limeunganishwa kwenye mzabibu, linazaa tunda. Tawi ambalo halijaunganishwa na mzabibu linakufa na haliwezi kuzaa matunda. Yesu aliwataka wanafunzi Wake daima kukaa karibu Naye kwa kupendana na kutii amri Zake.

Yohana 15:4–12

Yesu na Mitume Wake wakitembea kwenda Gethsemane.

Baada ya kufundisha mambo haya, Yesu na Mitume Wake waliimba wimbo. Walitembea kuelekea bustani iitwayo Gethsemane.

Mathayo 26:30