1 Wakorintho 12–13
Paulo Analinganisha Kanisa na Mwili wa Kristo
Akifundisha kuhusu karama za roho, umoja, na hisani
Korintho ulikuwa mji mkubwa, wenye shughuli nyingi. Waumini wengi wa Kanisa la Yesu Kristo waliishi huko. Lakini wote walikuwa kutoka maeneo tofauti na walikuwa tofauti sana na kila mmoja. Paulo alitaka kuwasaidia wawe na umoja na waone mema katika kila mmoja wao. Basi akawaandikia barua.
1 Wakorintho 1:11–13
Katika barua yake, Paulo aliwaambia Watakatifu kwamba wote walikuwa na karama maalum kutoka kwa Mungu. Baadhi ya watu walikuwa na karama ya imani. Wengine walikuwa na karama ya kufanya miujiza. Baadhi walikuwa na hekima, na wengine wangeweza kuwaponya wenzao. Baadhi ya watu waliweza kuzungumza lugha zingine. Watakatifu wote walikuwa na karama tofauti, lakini zote zilitoka kwa Mungu.
1 Wakorintho 12:311, 29–30
Paulo alifundisha kwamba ingawa Watakatifu walikuwa tofauti na kila mmoja, imani yao katika Yesu iliwaleta pamoja. Walipoamua kufuata mafundisho ya Yesu, kubatizwa, na kujiunga na Kanisa Lake, walikuwa kundi moja, lililoungana katika Yesu Kristo.
1 Wakorintho 12:27
Paulo alisema kwamba Kanisa ni kama mwili, wenye kichwa, mikono, miguu, na nyayo. Kila sehemu ya mwili hufanya vitu tofauti. Sikio halipaswi kujisikia vibaya kwa sababu liko tofauti na jicho. Na kichwa hakiwezi kusema kwa miguu, “Sina haja na wewe.” Kila sehemu ni muhimu, na vyote vinafanya kazi pamoja.
1 Wakorintho 12:12–14
Paulo aliwaita Watakatifu huko Korintho “mwili wa Kristo.” Aliwataka wafanye kazi pamoja kama sehemu tofauti za mwili, wakitumia karama zao tofauti ili kusaidiana na kubarikiana.
1 Wakorintho 12:15–27
Ili kufanya hivi, watu walihitaji aina maalum ya upendo, inayoitwa hisani. Ni upendo ambao Yesu Kristo anao kwa kila mtu. Paulo alisema kuwa na hisani inamaanisha kuwa na subira kwa wengine, hata kama wao siyo wakarimu. Inamaanisha kutokuwa mjeuri, mbinafsi, au mwenye wivu. Inamaanisha kuupenda ukweli na kuwa na tumaini.
1 Wakorinto 13: 1–7; Moroni 7:47.
Paulo aliwaambia Watakatifu huko Korintho kwamba hisani hudumu milele. Bila kujali karama gani nyingine tunazoweza kuwa nazo, sote tunahitaji kuwa na hisani. Yeyote kati yetu anaweza kuwa na hisani kama tutamwomba Baba wa Mbinguni kwa mioyo yetu yote na kujaribu kuwa wafuasi wa kweli wa Yesu Kristo.
1 Wakorinto 13:1–3, 8; Moroni 7:48.