Hadithi za Maandiko
Mfano wa Mtumishi Ambaye Hangesamehe—Yesu anafundisha kuhusu msamaha


Mathayo 18:21–34

Mfano wa Mtumishi Ambaye Hangesamehe

Yesu Anafundisha kuhusu msamaha

Petro anamuuliza Yesu swali.

Siku moja, Petro alimuuliza Yesu swali muhimu. Alitaka kujua ni mara ngapi anapaswa kuwasamehe watu wanapotenda dhambi. “Mara saba?” Petro aliuliza. Yesu alijibu swali la Petro kwa kumsimulia hadithi au fumbo.

Mathayo 18:15–21

Mtumishi anadaiwa fedha na mfalme.

Katika hadithi, kulikuwa na mfalme aliyekuwa na watumishi wengi. Mmoja wa watumishi alidaiwa na mfalme talanta elfu kumi. Hiyo ilikuwa fedha nyingi sana!

Mathayo 18:23–24

Yule mtumishi hawezi kulipa lile deni.

Mtumishi hangeweza kamwe kumlipa mfalme. Mfalme alisema kwamba angemuuza mtumishi na familia yake ili kulipa deni.

Mathayo 18:25

Mtumishi anaomba msamaha.

Mtumishi aliposikia haya, alipiga magoti. Alimwomba mfalme kumpa muda zaidi. “Nivumilie,” alisema, “nami nitakulipa yote pia.”

Mathayo 18:26

Mfalme anamsamehe mtumishi.

Mfalme alikuwa na huruma kwa mtumishi. Aliamua kumsamehe. Mtumishi hakuwa na haja ya kulipa fedha hizo. Alikuwa huru kwenda!

Mathayo 18:27

Mtumishi huyo anadai pesa kutoka kwa mtu mwingine.

Kisha mtumishi akaenda na kumpata mtu aliyemdai kiasi kidogo cha fedha. Alimshika mtu yule na kusema, “Nilipe.”

Mathayo 18:28

Mtu yule anamwomba mtumishi msamaha.

Mtu yule alipiga magoti. “Nivumilie,” alisema, “nami nitakulipa yote pia.” Lakini mtumishi hakumsamehe. Alimtupa gerezani.

Mathayo 18:29–30

Mfalme anamwambia mtumishi kuhusu msamaha.

Wakati mfalme alipogundua kilichotokea, aliomba kumwona yule mtumishi. Mfalme alimkumbusha mtumishi wake kwamba alikuwa amesamehewa deni kubwa sana. Alimwambia mtumishi wake kwamba alipaswa pia kumsamehe mtu aliyemdai pesa.

Mathayo 18:31–33

Yesu akizungumza na Petro kuhusu msamaha.

Sote tunadaiwa deni ambalo kamwe hatungeweza kujilipia wenyewe. Yesu alimwelezea Petro kwamba Mungu hutusamehe, hivyo pia tunapaswa kuwasamehe wengine. Na hatupaswi kuacha baada ya mara saba lakini tunapaswa daima kuwa tayari kusamehe.

Mathayo 18:22, 34–35; ona pia Mathayo 6:14; Mafundisho na Maagano 64:9–10