Warumi 3:21–28; 5:1–11; 6:3–6
Kumtegemea Yesu Kristo kwa ajili ya Wokovu
Kuokolewa kwa neema Yake
Watu kutoka sehemu nyingi tofauti walikuwa wakijiunga na Kanisa la Yesu Kristo. Waumini wa Kanisa waliitwa Watakatifu.
Warumi 1:7
Baadhi ya Watakatifu walikuwa Wayahudi ambao bado walifuata sheria ya Musa. Wengine hawakuifuata. Hawakukubaliana kuhusu ikiwa walihitaji kuifuata sheria ya Musa.
Warumi 2:14–15, 23–29
Paulo alijua kwamba Watakatifu walikuwa na maswali haya. Aliandika barua kwa Watakatifu huko Rumi. Aliwaambia kwamba hakuna anayeweza kuokolewa kwa kujaribu tu kuifuata sheria ya Musa. Sisi sote tunatenda dhambi, alieleza. Ili kuokolewa, kila mtu anahitaji kuwa na imani katika Yesu Kristo na kumfuata Yeye.
Warumi 3:20–23
Paulo alifundisha kwamba Mungu alimtuma Yesu Kristo ili ajichukulie juu Yake dhambi zetu. Kwa sababu ya dhabihu ya Yesu, sote tunaweza kutubu na kusamehewa dhambi zetu.
Warumi 3:24–31
Paulo alifundisha kwamba Yesu Kristo anatupatia zawadi ya msamaha na nguvu ya kufanya mambo mema. Zawadi hii ya upendo inaitwa neema ya Yesu Kristo, na inatujaza kwa tumaini na shangwe. Paulo alisema kwamba tunapobatizwa, kama Yesu alivyobatizwa, ni kama kuanza maisha mapya kama mfuasi wa Yesu.
Warumi 5:1–11; 6:3–6