Yohana 10:1–18
Yesu Ndiye Mchungaji Mwema
"Kondoo wangu waisikia sauti yangu, nami nawajua"
Yesu aliwaambia watu katika Yerusalemu kwamba Yeye ni kama mchungaji mwema. Wanafunzi Wake, au wafuasi Wake, ni kama kondoo Wake. Mchungaji mwema anawapenda kondoo wake. Yeye anajua jina la kila mmoja.
Yohana 10:3, 14; ona pia Helamani 15:13
Kondoo wanaijua sauti ya mchungaji mwema. Anapowaita, wanasikia na kutii.
Yohana 10:4, 27
Mchungaji mwema huwatunza kondoo wake. Anawaongoza kwenye malisho ya kijani, kama vile Yesu Kristo anavyotuongoza kwenye uzima wa milele.
Yohana 10:9–10, 28
Wakati mtu mwingine anapoajiriwa kuwatunza kondoo, hawamfuati, kwa sababu hawajui sauti yake. Hatari inapokuja, mtu aliyeajiriwa hukimbia. Hawajali kondoo kama mchungaji mwema anavyowajali.
Yohana 10:5, 12–13
Mchungaji mwema hakimbia wakati kuna hatari. Anabaki kuwalinda kondoo Wake. Yeye yuko tayari hata kutoa maisha yake kwa ajili yao, kama vile Yesu Kristo alivyotoa uhai Wake kwa ajili yetu ili tuweze kuwa na uzima wa milele.
Yohana 10:11, 17–18
Yesu aliwaambia watu huko Yerusalemu kwamba Yeye pia alikuwa na kondoo wengine ambao waliishi katika sehemu zingine. Yesu alisema Yeye angewatembelea pia, na wangesikia mafundisho Yake. Kitabu cha Mormoni kinasimulia kuhusu Yesu akiwatembelea baadhi ya kondoo Wake wengine katika Amerika.
Yohana 10:16; 3 Nefi 15:11–24