Marko 2:1–12
Yesu Anamponya Mtu Ambaye Hakuweza Kutembea
Uponyaji wa kimwili na kiroho
Watu wengi walitaka kumsikia Yesu akifundisha. Siku moja Yeye alikuwa katika nyumba iliyojaa watu.
Marko 2:1–2
Watu wanne walikuja kwenye nyumba na rafiki ambaye hakuweza kutembea. Iliwabidi wambebe kitandani. Walitaka kumleta rafiki yao kwa Yesu, lakini nyumba ilikuwa imejaa msongamano, hawakuweza kuingia.
Marko 2:3–4
Kwa hivyo walimbeba rafiki yao hadi kwenye paa la nyumba. Walitoa sehemu ya paa na kumshusha rafiki yao na kitanda chake ndani ya nyumba, katikati ya umati wa watu, mbele ya Yesu.
Marko 2:4
Naye Yesu, alipoiona imani yao, akamwambia yule mwenye kupooza, “Mwanangu, umesamehewa dhambi zako.”
Marko 2:5
Baadhi ya viongozi wa Wayahudi, waliposikia haya, walikasirika. Walifikiri kwamba ni Mungu pekee angeweza kusamehe dhambi.
Marko 2:6–7
Yesu alijua kile walichokuwa wakifikiria. Ili kuwasaidia kuelewa kwamba alikuwa na uwezo wa kusamehe dhambi, Yeye alifanya muujiza. Yeye alimwambia mtu ambaye hakuweza kutembea, “Ondoka, ujitwike godoro lako uende nyumbani kwako.” Mtu yule alisimama na kutembea! Kila mtu alishangazwa na kutoa shukrani kwa Mungu.
Marko 2:8–12