Luka 19:1–10
Zakayo Mtoza Ushuru
Akipanda mti kumwona Yesu
Yesu alitembelea mji wa Yeriko. Mtu aliyeitwa Zakayo aliishi huko. Zakayo alikuwa mtoza ushuru tajiri. Watu wengi hawakuwapenda watoza ushuru. Walifikiri watoza ushuru walichukua pesa nyingi sana kutoka kwa watu.
Luka 19:1–2
Zakayo alisikia kwamba Yesu alikuwa mjini. Alitaka kujifunza zaidi kumhusu Yeye. Alijaribu kwenda kumwona Yesu, lakini hakuweza kwa sababu kulikuwa na watu wengi waliomzunguka, na Zakayo alikuwa mfupi sana kuona juu yao. Ni kwa jinsi gani angepata kumwona Yesu?
Luka 19:3–4
Zakayo alikimbia mbele na kupanda mti ili aweze kumwona Yesu. Wakati Yesu alipopita, Yeye alitazama juu na kumwona Zakayo kwenye mti. Yesu aliita jina lake na kusema, "Shuka chini." Yesu alitaka kumtembelea nyumbani kwake. Zakayo aliharakisha kushuka mtini. Alikuwa na furaha sana kuweza kupata Yesu aje nyumbani kwake.
Luka 19:4–6
Watu katika Yeriko walijiuliza kwa nini Yesu angeenda nyumbani kwa Zakayo. Walidhani Zakayo alikuwa mwenye dhambi kwa sababu alikuwa mtoza ushuru.
Luka 19:7
Zakayo alimwambia Yesu, "Nusu ya mali yangu nawapa maskini." Alisema kwamba kama angechukua pesa nyingi sana kutoka kwa mtu fulani, angewarudishia hata zaidi. Yesu alimwambia Zakayo, "Leo wokovu umefika nyumbani humu." Yesu alisema alikuwa amekuja kuwatafuta na kuwaokoa watu waliopotea.
Luka 19:6, 8–10