Hadithi za Maandiko
Yesu Anatuliza Dhoruba—Hata upepo na bahari vinamtii Yeye


Mathayo 8:23–27; Marko 4:36–41

Yesu Anatuliza Dhoruba

Hata upepo na bahari vinamtii Yeye

Yesu na wanafunzi Wake ndani ya mashua.

Siku moja, Yesu na wanafunzi Wake walikuwa wanasafiri katika mashua kwenye Bahari ya Galilaya. Upepo ulianza kuvuma kwa nguvu sana. Mawimbi yalianza kupiga ndani ya mashua, yakiijaza maji. Yesu, hata hivyo, alikuwa amelala kwa amani.

Mathayo 8:23–24

Wanafunzi wanamwamsha Yesu.

Wanafunzi waliogopa. Walimwamsha Yesu. “Bwana, tuokoe,” walilia. Walidhani kuwa watazama baharini.

Mathayo 8:25

Yesu anaamuru maji yatulie.

“Mbona mmekuwa waoga?” Yesu aliuliza. Yeye aliwaambia wanafunzi kwamba walihitaji kuwa na imani zaidi. Kisha alisimama na kuuambia upepo na mawimbi, “Nyamaza, na utulie.”

Mathayo 8:26; Marko 4:39

Wanafunzi wakijiuliza ni kwa jinsi gani Yesu angeweza kutuliza dhoruba.

Ghafla upepo ulikoma, na bahari ikawa shwari. Yesu na wanafunzi walikuwa salama. Wanafunzi wa Yesu walishangazwa. Walishangaa ni mtu wa nama gani anayeweza kuamuru upepo na bahari, na vikamtii Yeye!

Mathayo 8:26–27