Hadithi za Maandiko
Utangulizi: Kuhusu Agano Jipya—Hadithi ya Yesu Kristo na wafuasi Wake


Utangulizi

Kuhusu Agano Jipya

Hadithi ya Yesu Kristo na wafuasi Wake

Nabii wa kale akiandika kwenye karatasi ya ngozi.

Biblia ina sehemu mbili: Agano la Kale na Agano Jipya. Agano la Kale lina maandishi ya manabii kutoka zamani za kale. Baadhi ya manabii hawa waliandika kwamba Mungu aliahidi kumtuma Mwokozi. Yeye angekuwa Mwana wa Mungu na kutuokoa kutokana na dhambi na kifo ili tuweze kuishi na Mungu tena.

Isaya 53:3–5; Yakobo 7:11; Musa 4

Mariamu akiwa amembeba mtoto Yesu.

Agano Jipya linaelezea kuhusu jinsi ahadi hii ilivyotimizwa. Linasimulia kuhusu kuzaliwa kwa Yesu Kristo, Mwana wa Mungu.

Luka 2:4–7

Yesu akifundisha kikundi cha watu.

Agano Jipya pia linaelezea kuhusu maisha ya Yesu. Yeye aliishi miongoni mwa Wayahudi na alitufundisha jinsi ya kuishi ili tuweze kurudi kwa Baba wa Mbinguni siku moja.

Mathayo 5:1–2

Yesu akimhudumia mtoto.

Yesu aliwabariki na kuwahudumia watu. Yeye alifanya miujiza mingi kwa ajili yao, kama vile kuwaponya watu ambao walikuwa wagonjwa na kuwafanya wafu kuwa hai.

Mathayo 4:23

Yesu akimtawaza mmoja wa Mitume Wake.

Yesu aliwachagua kumi na wawili wa wafuasi Wake kuwa Mitume. Yeye aliwapa wao mamlaka ya kuliongoza Kanisa Lake.

Luka 9:1–2

Yesu akiibuka kutoka kaburini

Kwa sababu Yeye anatupenda, Yesu alijichukulia juu Yake Mwenyewe maumivu yetu yote, huzuni, na dhambi. Yeye alikufa kwa ajili yetu. Kisha, siku tatu baadaye, Yeye alishinda kifo na akafufuka! Yesu Kristo yu hai na kwa sababu Yake, tunaweza kutubu dhambi zetu na kuishi tena baada ya kufa.

Alma 7:11–13

Watoto wawili wa siku za leo wakisoma Agano Jipya.

Watu waliomjua na kumpenda Yesu waliandika kuhusu haya yote. Mitume Wake waliandika barua ili kuwasaidia waumini wa Kanisa kujenga imani yao katika Yesu Kristo. Mambo waliyoyaandika yamehifadhiwa kwa miaka mingi, mingi sana. Sasa unaweza kuyasoma katika Agano Jipya na kujifunza jinsi ya kumfuata Yesu Kristo.

Luka 1:1–4