Hadithi za Maandiko
Hakuna Kinachoweza Kututenganisha na Upendo wa Kristo—Ahadi kwa nyakati ambapo maisha ni magumu


Warumi 8:18–39

Hakuna Kinachoweza Kututenganisha na upendo wa Kristo

Ahadi kwa nyakati ambapo maisha ni magumu

Paulo akiandika barua kwa Warumi. Muumini wa Kanisa akitendewa vibaya.

Rumi ulikuwa mji mkubwa sana wenye watu wengi. Baadhi ya watu walikuwa wafuasi wa Yesu Kristo, lakini wengi hawakuwa. Watu wengi katika Rumi waliamini katika vitu ambavyo vilikuwa tofauti sana na kile Yesu alichofundisha. Wakati mwingine watu huko Rumi waliwatendea waumini wa Kanisa mambo yasiyo ya ukarimu.

Muumini wa Kanisa akisali na kupokea mwongozo wa kiungu.

Mtume Paulo aliandika barua kwa Watakatifu huko Rumi. Aliwataka wajue kwamba japokuwa maisha wakati mwingine ni magumu, Mungu alikuwa na baraka kuu za kuwapa. Kama tunampenda Mungu, Yeye anaweza kusaidia mambo magumu katika maisha yetu kuongoza kwenye kitu kilicho kizuri.

Warumi 8:18, 28

Muumini wa Kanisa akimsaidia mtu ambaye alikuwa si mwema kwake.

Paulo aliandika kwamba hakuna kinachoweza kututenganisha na upendo wa Yesu Kristo. Bila kujali changamoto zetu ni ngumu kiasi gani, Yeye anaweza kutusaidia kuzivuka.

Warumi 8:31, 35–39