Hadithi za Maandiko
Yohana Mbatizaji Anazaliwa—Mungu anatimiza ahadi kwa Elisabeti na Zakaria


Luka 1:5–25, 57–80

Yohana Mbatizaji Anazaliwa

Mungu anatimiza ahadi kwa Elisabeti na Zakaria

Zakaria na Elisabeti wakisali ili kupata mtoto.

Zakaria na Elisabeti walikuwa watu waaminifu ambao walimpenda Mungu. Walisali ili kupata mtoto. Sasa walikuwa wazee sana, na bado hawakuwa na watoto.

Luka 1:5–7

Zakaria akihudumu katika hekalu.

Zakaria alikuwa kuhani aliyehudumu katika hekalu huko Yerusalemu. Siku moja, alichaguliwa kuchoma uvumba katika chumba kitakatifu hekaluni.

Luka 1:8–10

Malaika akimtokea Zakaria.

Ghafla, malaika alitokea. Zakaria aliogopa. Malaika alisema, “Usiogope, Zakaria: maana sala yako imesikilizwa.” Yeye alisema Zakaria na Elisabeti wangepata mtoto wa kiume. Walipaswa kumwita Yohana. Malaika alisema kwamba Yohana alikuwa na kazi muhimu ya kufanya. Angewasaidia watu kujiandaa kumpokea Mwokozi wakati Yeye atakapokuja.

Luka 1:12–17

Zakaria akizungumza na malaika.

Zakaria hakuweza kuamini kile malaika alichokuwa akisema. Yeye na Elisabeti walikuwa wazee sana kupata watoto. Malaika alisema kwamba kwa sababu Zakaria hakuamini ujumbe wake, asingeweza kuzungumza hadi Yohana atakapozaliwa.

Luka 1:18–20

Zakaria akiondoka hekaluni. Hakuweza kuzungumza.

Watu walishangaa kwa nini Zakaria alikuwa anachukua muda mrefu ndani ya hekalu. Alipokuwa akiondoka, hakuweza kuzungumza. Waliweza kujua kitu maalum kilikuwa kimetokea.

Luka 1:21–23

Elisabeti na Zakaria wakiwa wamembeba mtoto wao aliyezaliwa.

Miezi kadhaa baadaye, Elisabeti alipata mtoto, kama vile malaika alivyoahidi. Familia yao na marafiki walikuwa na furaha sana! Walikuja kukutana na mtoto.

Luka 1:57–59

Elisabeti na Zakaria wakimpa mtoto jina.

Walidhani mtoto alipaswa kuitwa Zakaria, kama baba yake. Elisabeti alisema, “Ataitwa Yohana.” Walimwuliza Zakaria, ambaye bado hakuweza kuzungumza. Aliandika, “Jina lake ni Yohana.” Kila mtu alishangaa.

Luka 1:59–63

Zakaria akisema kwamba mtoto atakuwa nabii.

Ghafla, Zakaria aliweza kuzungumza tena. Alimshukuru Mungu na alikuwa amejawa na Roho Mtakatifu. Alimwambia kila mtu kwamba Mungu alikumbuka ahadi Zake kwa watu Wake. Alisema kwamba Yohana angekuwa nabii. Yohana angewafundisha watu kutubu na kubatizwa. Angewasaidia wao kujiandaa kujifunza kutoka kwa Yesu Kristo.

Luka 1:64–80