Marko 10:13–16
Yesu Anawabariki Watoto wadogo
“Kwa maana watoto kama hawa ufalme wa Mungu ni wao”
Wakati Yesu alipokuwa akifundisha, baadhi ya watu waliwaleta watoto wao wadogo Kwake. Walimtaka Yesu awabariki watoto wao. Wanafunzi Wake walijaribu kuwakataza.
Mathayo 19:13; Marko 10:13
Yesu aliwaambia wanafunzi wawaache watoto waje Kwake. Yeye alisema kwamba watoto wadogo ni wa ufalme wa Mungu. Yeye alielezea kwamba kama mtu anataka kuishi na Mungu tena, anahitaji kuwa kama mtoto mdogo.
Mathayo 19:14; Marko 10:14–15
Kisha Yesu aliwachukua watoto wadogo mikononi Mwake na kuwabariki.
Mathayo 19:15; Marko 10:16