Yohana 4
Yesu, Mwanamke, na Kisima
Akifundisha kuhusu maji ya uzima
Yesu na wanafunzi Wake walikuwa wakitembea kupita Samaria wakielekea Galilaya. Walisimama ili kupata maji kisimani. Wakati Yesu akipumzika hapo, wanafunzi Wake walikwenda kununua chakula.
Yohana 4:3–8
Mwanamke kutoka Samaria alikuja kisimani kujaza mtungi wake wa maji. Yesu alimwomba maji ya kunywa. Mwanamke alishangaa. Yesu alikuwa Myahudi, na Wayahudi wengi hawakuzungumza na Wasamaria.
Yohana 4:7–9
Yesu alimwambia kwamba watu wanaokunywa maji kutoka kisimani wanapata kiu tena. Lakini angeweza kumpa “maji ya uzima” ya uzima wa milele, na asingeona kiu kamwe. Mwanamke huyo alisema alitaka kiasi cha “maji haya ya uzima.”
Yohana 4:10–14
Yesu alimwambia akamlete mumewe. “Sina mume,” alisema. Yesu alimwambia alikuwa na waume watano, na mtu aliyeishi naye hakuwa mumewe.
Yohana 4:16–18
Mwanamke alishangaa kwamba Yesu alijua mambo haya kumhusu. Alisema alijua kwamba Mwokozi alikuwa anakuja punde. Yesu alimwambia kwamba Yeye ni Mwokozi.
Yohana 4:19, 25– 25
Mwanamke aliuacha mtungi wake wa maji kisimani na kwenda mjini. Aliwaambia watu wengi kwamba alikuwa amempata Mwokozi. Aliwaalika kuja na kumsikiliza Yeye akifundisha. Kwa sababu ya mwanamke huyu, Wasamaria wengi waliamini katika Yesu Kristo.
Yohana 4:28–29, 39–42