Marko 8:22–25
Yesu Anamponya Kipofu
Uponyaji ambao hutokea baada ya muda
Katika mji ulioitwa Bethsaida, watu walimleta kipofu kwa Yesu. Walitaka Yesu ambariki ili aweze kuona.
Marko 8:22
Yesu aliushika mkono wa mtu huyo na kumwongoza kutoka nje ya mjini. Kisha Yesu akamwekea mtu huyo mikono yake na kumbariki.
Marko 8:23
Yesu alimuuliza mtu yule kama ameeweza kuona kitu cho chote. Mtu huyo alitazama juu. Alisema aliweza kuona kidogo, lakini sio wazi kabisa. Alisema kwamba watu walionekana kama miti inayotembea.
Marko 8:23–24
Yesu alimbariki mtu yule tena. Wakati huu, alipotazama juu, kila kitu kilikuwa wazi. Yesu alikuwa amemponya!
Marko 8:25