Matendo ya Mitume 9:36–42
Tabitha, Mwanamke “Aliyejaa Matendo Mema”
Alifufuliwa kwa uwezo wa Yesu Kristo
Tabitha alikuwa mwanafunzi mwaminifu wa Yesu Kristo. Aliishi katika mji kando ya bahari, uitwao Yafa. Alipenda kuwahudumia na kuwasaidia watu waliokuwa masikini.
Matendo ya Mitume 9:36
Tabitha alitengeneza nguo na kuwapa wanawake walio katika shida. Walimpenda Tabitha.
Matendo ya Mitume 9:39
Siku moja, Tabitha alikuwa mgonjwa sana. Alikuwa mgonjwa sana kiasi kwamba alikufa.
Matendo ya Mitume 9:37
Waumini wengine wa Kanisa huko Yafa walihuzunika sana. Walijua kwamba Petro, mmoja wa Mitume wa Yesu, alikuwa katika mji uliokuwa karibu. Waliwatuma watu wawili kumwomba Petro aje kwao haraka.
Matendo ya Mitume 9:38
Petro alikuja pale mwili wa Tabitha ulipokuwepo. Baadhi ya wanawake waliosaidiwa na Tabitha walikuwepo pale. Walimwonyesha Petro nguo alizozitengeneza kwa ajili yao.
Matendo ya Mitume 9:39
Petro aliwaomba watu wote kuondoka chumbani. Alipiga magoti na kusali.
Matendo ya Mitume 9:40
Baada ya kusali, Petro alisema, “Tabitha, inuka.” Alifungua macho yake na akaketi kitako. Petro alimsaidia Tabitha kusimama. Alikuwa hai tena! Petro aliwaita marafiki zake waje na kumwona. Walistaajabu! Walijua alikuwa amefufuliwa kwa nguvu ya Yesu Kristo. Watu wengi zaidi walimwamini Yesu.
Matendo ya Mitume 9:40–42