Hadithi za Maandiko
Yesu Anamponya Mtumishi wa Akida—Kiongozi wa Kirumi aonyesha imani kubwa


Luka 7:1–10

Yesu Anamponya Mtumishi wa Akida

Kiongozi wa Kirumi aonyesha imani kubwa

Akida pamoja na askari wake.

Akida aliishi Kapernaumu, mji ambao Yesu mara nyingi alifundisha. Alikuwa kiongozi wa kundi kubwa la askari.

Luka 7:1–2

Mtumishi wa akida ni mgonjwa sana.

Akida huyu alikuwa na mtumishi ambaye alikuwa wa kipekee kwake. Mtumishi akawa mgonjwa na alikuwa anaenda kufa.

Luka 7:2.

Akida anawaomba baadhi ya viongozi wa Kiyahudi kumtafuta Yesu.

Ingawa akida hakuwa Myahudi, alikuwa amesikia juu ya Yesu. Aliamini kwamba Yesu alikuwa na uwezo wa kufanya miujiza mikubwa. Aliwatuma baadhi ya viongozi wa Wayahudi kumwomba Yesu aje kumponya mtumishi wake.

Luka 7:3–4

Baadhi ya watu wanamwambia Yesu asiende nyumbani kwa akida.

Viongozi walimwambia Yesu kuhusu akida na mtumishi wake. Walisema kwamba akida huyu alikuwa mkarimu kwa Wayahudi. Yesu alianza kutembea kuelekea nyumba ya akida. Lakini kabla hajafika huko, baadhi ya marafiki wa akida walimsimamisha Yesu. Walimwambia Yeye asiingie ndani ya nyumba.

Luka 7:4–6

Watu wanamwambia Yesu kwamba akida hakuhisi kustahili.

Marafiki walisema kwamba akida hakuhisi kustahili kuwa na Yesu katika nyumba yake. Aliamini kwamba Yesu angeweza kumponya mtumishi wake hata kutokea mbali sana!

Luka 7:6–8

Yesu anasema kwamba akida ana imani kubwa.

Yesu alishangazwa na imani ya akida. Alisema kwamba hakuwa ameona imani kubwa kama hiyo.

Luka 7:9.

Mtumishi wa akida anaponywa.

Wakati marafiki wa akida waliporudi nyumbani kwake, mtumishi alikuwa ameponywa kabisa. Yesu alikuwa amemponya, kama vile akida alivyoamini kuwa Yeye angeweza kumponya.

Luka 7:10