Hadithi za Maandiko
Paulo na Sila—Waliokolewa kwa miujiza kutoka kwa Bwana


Matendo ya Mitume 16:9–40

Paulo na Sila

Waliokolewa kwa miujiza kutoka kwa Bwana

Paulo na Sila wakisafiri pamoja.

Bwana aliwaita Paulo na Sila kuihubiri injili pamoja. Walisafiri kwenda miji mingi ili kuona jinsi makanisa yalivyokuwa yakiendelea.

Matendo ya Mitume 15:40–41; 16:4–8

Paulo anapata ono.

Usiku mmoja, katika ono, Paulo alimwona mtu kutoka Makedonia akimwomba aje kwenye mji wake. Paulo na Sila waliondoka mara moja. Walijua Mungu aliwataka waende.

Matendo ya Mitume 16:9–10

Paulo na Sila wakimhubiria mwanamke aliyeitwa Lidia.

Walipofika Makedonia, mwanamke aliyeitwa Lidia aliwasikia wakifundisha. Bwana alifungua moyo wa Lidia. Aliamini kile Paulo alichofundisha na akabatizwa.

Matendo ya Mitume 16:13–15

Lidia anawaambia Paulo na Sila kwamba wanaweza kukaa nyumbani mwake.

Lidia aliwaambia Paulo na Sila kwamba wangeweza kukaa nyumbani mwake wakati wakiwa huko.

Matendo ya Mitume 16:15

Watu wanawapeleka Paulo na Sila mahali pa soko.

Lakini si kila mtu alipenda kwamba Paulo na Sila walikuwa pale. Baadhi ya watu hawakupenda kile walichokuwa wakikifundisha. Waliwapeleka Paulo na Sila sokoni na kuwaambia viongozi wa mji kwamba walikuwa wakisababisha matatizo.

Matendo ya Mitume 16:16–21

Watu wamewakasirikia Paulo na Sila.

Watu waliwakasirikia Paulo na Sila. Viongozi wa mji walichana nguo za Paulo na Sila na kusema kwamba walipaswa kupigwa.

Matendo ya Mitume 16:22–23

Paulo na Sila wakiwekwa gerezani.

Kisha viongozi wa mji waliwatupa Paulo na Sila gerezani. Waliwafunga miguu yao na kuwawekea ulinzi.

Matendo ya Mitume 16:23–24

Kamba za gereza zilizowafunga Paulo na Sila zinalegezwa.

Usiku ule, Paulo na Sila walisali na kuimba nyimbo kwa Mungu wakati wafungwa wengine wakiwasikiliza. Ghafla, ardhi ilianza kutikisika. Milango ya gereza ilifunguliwa, na kamba zilifunguliwa.

Matendo ya Mitume 16:25–26

Paulo anamwambia mlinzi asiwe na shaka.

Mlinzi aliamka na kuona milango iko wazi. Alifikiri wafungwa walikuwa wamekimbia na kwamba angekuwa katika matatizo kwa kuwaacha wakimbie. Paulo alimwambia mlinzi asiwe na shaka. Wafungwa wote walikuwa bado wako pale.

Matendo ya Mitume 16:27–28

Paulo anamwambia mlinzi kuamini katika Yesu Kristo.

Mlinzi alikuwa na hofu. Alipiga magoti kando ya Paulo na Sila na kusema, “Ninapaswa nifanye nini ili niokolewe?” Walisema, “Mwamini Bwana Yesu Kristo.”

Matendo ya Mitume 16:27–31

Paulo na Sila wanafundisha injili kwa yule mlinzi na familia yake.

Paulo na Sila walimfundisha mlinzi na familia yake injili. Mlinzi alitibu majeraha ya Paulo na Sila. Usiku ule, yeye na familia yake walibatizwa.

Matendo ya Mitume 16:32–33