Matendo ya Mitume 8:5–24
Simoni na Nguvu za Mungu
Kujifunza kuhusu ukuhani wa Mungu
Mtu aliyeitwa Simoni aliishi huko Samaria. Aliposikia injili ya Yesu Kristo, aliamini. Pia alishangazwa na miujiza ambayo wanafunzi wa Yesu waliifanya kwa nguvu ya Mungu. Simoni alibatizwa, na vivyo hivyo wanaume na wanawake wengine wengi katika Samaria.
Matendo ya Mitume 8:5–13
Mitume huko Yerusalemu walisikia kwamba watu katika Samaria walikuwa wakibatizwa. Petro na Yohana walikwenda Samaria. Wakitumia nguvu za Mungu, ukuhani, waliweka mikono yao juu ya watu ambao walikuwa wamebatizwa na kuwapa kipawa cha Roho Mtakatifu.
Matendo ya Mitume 8:14–17
Wakati Simoni alipowaona Petro na Yohana wakifanya hivi, aliwapa pesa na kusema, “Nipeni na mimi uwezo huu.” Alitaka kununua ukuhani wa Mungu ili aweze kutoa kipawa cha Roho Mtakatifu pia.
Matendo ya Mitume 8:18–19
Petro alieleza kwamba hakuna mtu awezaye kununua nguvu za Mungu. Ni kipawa kutoka Kwake. Petro alimwambia Simoni kwamba moyo wake ulihitaji kubadilika. Alimwalika Simoni kutubu na kusali kwa Mungu kwa ajili ya msamaha.
Matendo ya Mitume 8:20–23
Simoni alisikitika. Alimwomba Petro asali kwa ajili yake ili amsaidie abadilike.
Matendo ya Mitume 8:24