Hadithi za Maandiko
Shetani Anamjaribu Yesu—Mfano wa kushinda majaribu


Mathayo 4:1–10

Shetani Anamjaribu Yesu

Mfano wa kushinda majaribu

Yesu akitembea nyikani.

Baada ya ubatizo Wake, Yesu alienda nyikani ili kuwa na Mungu. Hakula kwa siku 40. Alikuwa akifunga na kusali ili kujiandaa kwa ajili ya misheni Yake.

Mathayo 4:1–2; ona Tafsiri ya Joseph Smith katika muhtasari 1b na 2c

Shetani akimjaribu Yesu kugeuza mawe kuwa mkate.

Yesu alikuwa na njaa. Shetani alikuja na kumjaribu Yeye. Alisema kwamba kama Yesu alikuwa Mwana wa Mungu, angeweza kugeuza mawe kuwa mkate. Yesu asingefanya hivyo. Yesu alinukuu maandiko yanayosema kwamba Yeye aliishi kwa neno la Mungu, siyo mkate pekee.

Mathayo 4:2–4

Shetani akimjaribu Yesu kuruka kutoka juu ya kinara cha hekalu.

Kisha Roho Mtakatifu alimpeleka Yesu juu ya kinara cha hekalu. Shetani alimjaribu Yesu aruke. Alisema kwamba ikiwa Yesu alikuwa Mwana wa Mungu, malaika wasingemwacha Yeye aumie. Yesu hakuruka. Yeye alimwambia Shetani kwamba maandiko yanasema hatupaswi kumjaribu Mungu.

Mathayo 4:5–7; ona Tafsiri ya Joseph Smith katika muhtasari 5a na 6a

Shetani akimjaribu Yesu amwabudu yeye.

Kisha, Roho Mtakatifu alimpeleka Yesu kwenye kilele cha mlima. Kutoka hapo, Yesu angeweza kuona falme zote za ulimwengu. Shetani alikuja na kusema kwamba angempa Yesu falme hizi zote kama angemsujudia.

Mathayo 4:8–10; ona Tafsiri ya Joseph Smith 8a

Yesu akimwambia Shetani aondoke.

Yesu alimwambia Shetani kwamba maandiko yanasema tunapaswa kumsujudia Mungu pekee. Yesu alimwambia Shetani aondoke. Yesu alikwenda Galilaya kufundisha injili Yake. Yeye alijazwa na nguvu ya Roho Mtakatifu.

Luka 4:13–14