Hadithi za Maandiko
Yesu Anawaponya Wanaume Kumi Waliokuwa na Ukoma—Umuhimu wa shukrani


Luka 17:11–19

Yesu Anawaponya Wanaume Kumi Waliokuwa na Ukoma

Umuhimu wa shukrani

Yesu anaona kundi la wanaume ambao ni wagonjwa.

Yesu alipokuwa akisafiri, aliingia kijijini na kuwaona wanaume kumi ambao walikuwa na ugonjwa mbaya sana wa ngozi uitwao ukoma. Watu wenye ukoma walilazimika kukaa mbali na kila mtu, hata familia zao, hivyo hawakuwafanya watu wengine wawe wagonjwa.

Luka 17:11–12

Wanaume hawa walimwomba Yesu awaponye.

Wanaume hawa walimwita Yesu na kumwomba awaponye. Yesu aliwaambia waende kwa makuhani katika mji. Ni makuhani tu ndio wangeweza kuamua kama wangeweza kuwa na watu wengine tena.

Luka 17:13–14; ona pia Mambo ya Walawi 14:2–3

Wanaume wanaponywa.

Wanaume kumi wagonjwa walipokuwa wakitembea ili kuonana na makuhani, muujiza ulitokea. Ugonjwa wao ukatoweka. Walikuwa wameponywa!

Luka 17:14

Mmoja wa wanaume anamshukuru Mungu kwa kuponywa.

Wakati mmoja wa wanaume alipoona kwamba ameponywa, aligeuka na kumshukuru Mungu kwa sauti kubwa. Alikuwa Msamaria.

Luka 17:15–16

Yesu akizungumza na mtu yule kuhusu imani.

Mtu yule alianguka miguuni pa Yesu kumshukuru kwa kile alichokifanya. Yesu aliuliza wako wapi wale watu wengine tisa walioponywa. Ni mtu mmoja tu aliyekuwa amerudi kumshukuru Yeye! Yesu kisha akamwambia, “Inuka enenda zako, imani yako imekuponya.”

Luka 17:16–19