Hadithi za Maandiko
Yesu Anakamatwa—Kumhukumu Mwana wa Mungu


Marko 14–15; Luka 22–23; Yohana 18–19

Yesu Anakamatwa

Kumhukumu Mwana wa Mungu

Yuda na baadhi ya walinzi wakiwasili Gethsemane.

Baada ya Yesu kumaliza kusali na kuteseka Gethsemane, Yuda aliwasili na kundi kubwa la walinzi wa Kiyahudi. Yuda alikuwa mmoja wa Mitume. Alijua kwamba Yesu mara kwa mara alienda kwenye bustani hii. Viongozi wa Kiyahudi walikuwa wamemlipa Yuda ili awasaidie kumpata Yesu ili waweze kuondoka Naye.

Yohana 18:2–3

Petro anamshambulia mtumishi wa kuhani mkuu.

Walinzi walipojaribu kumtwaa Yesu, Petro alichomoa upanga. Alikata sikio la mtumishi wa kuhani mkuu.

Yohana 18:10

Yesu anamwambia Petro aweke kando upanga wake.

Yesu anamwambia Petro aweke kando upanga wake. Yesu alisema kwamba Yeye alihitaji kufanya kile Baba Yake alichotaka.

Yohana 18:11

Yesu anaponya sikio la mtumishi.

Yesu aligusa sikio la mtumishi na kuliponya.

Luka 22:51

Yesu anapelekwa kwenye nyumba ya kuhani mkuu.

Walinzi walimpeleka Yesu kwenye nyumba ya kuhani mkuu. Viongozi wengine wa Kiyahudi walikuwa huko pia. Walitaka kutafuta sababu ya Yesu kuuawa. Walileta watu ndani ili kusimulia uongo kumhusu Yeye.

Marko 14:53–61

Kuhani mkuu anamwuliza Yesu kama Yeye ni Mwana wa Mungu.

Mwishowe, kuhani mkuu alimwuliza Yesu kama alikuwa Mwana wa Mungu. Yesu alisema, "Mimi Ndiye"

Marko 14:61–62

Kuhani mkuu na viongozi wengine wanamkasirikia Yesu.

Hili liliwafanya kuhani mkuu na viongozi wengine wakasirika. Walimpiga Yesu, wakamtemea mate, na kumfanyia Yeye mzaha. Walikubali kwamba Yeye alipaswa auwawe.

Marko 14:63–65

Petro anawaambia watu kwamba yeye hamjui Yesu.

Wakati Yesu alipokuwa katika nyumba ya kuhani mkuu, Petro alisubiri nje. Aliketi karibu na moto ili kujipasha joto. Mara tatu, watu walisema walimtambua Petro kama mmoja wa wanafunzi wa Yesu. Lakini kila wakati, Petro alisema hakumjua Yesu.

Marko 14:54, 66–71

Petro anaondoka akilia.

Kisha jogoo akawika, na Petro akakumbuka kile Yesu alichosema: kwamba Petro angemkana mara tatu. Petro alitembea akilia.

Marko 14:72

Viongozi Wayahudi wanampeleka Yesu kwa Pilato.

Viongozi Wayahudi walimpeleka Yesu kwa Pilato, gavana wa Kirumi. Umati wa watu ulikuja pia. Viongozi walimtaka Pilato atoa amri Yesu kuuawa. Walimwambia Pilato kwamba Yesu alijiita Mfalme wa Wayahudi.

Marko 15:1–3; Luka 23:2; Yohana 18:28–31

Yesu anazungumza na Pilato.

Pilato alimwuliza Yesu kama alikuwa mfalme wa Wayahudi. Yesu alisema, "Ufalme wangu si wa ulimwengu huu." Yeye alielezea kwamba Yeye alikuja ulimwenguni kuwafundisha watu ukweli.

Yohana 18:33–37

Yesu na Pilato wanasimama mbele ya umati.

Pilato alisema kwamba hakuamini Yesu alikuwa amefanya kosa lolote. Lakini watu wengi walipiga kelele, "Msulubishe." Pilato aliamua kufanya kile walichotaka na amuacha Yesu kuuawa.

Marko 15:12–14; Luka 23:14–24