Matendo ya Mitume 6–7
Stephano anashuhudia juu ya Yesu Kristo
Mtumishi jasiri anayeutoa uhai wake kwa ajili ya ushuhuda wake
Kanisa lilikuwa linakua haraka. Ilikuwa ni vigumu sana kwa Mitume kuwachunga waumini wote.
Matendo ya Mitume 6:1–2
Mitume waliamua kuwaita wanaume saba ambao wangeweza kusaidia. Waliwaomba waumini kuwatafuta wanaume ambao walikuwa na hekima na waliojawa Roho Mtakatifu.
Matendo ya Mitume 6:3
Mmoja wa watu waliowachagua alikuwa Stefano. Mitume walimpa baraka. Stefano alikuwa na imani kubwa na alifanya miujiza mikubwa miongoni mwa watu.
Matendo ya Mitume 6:5–8
Stefano alifundisha kuhusu Yesu Kristo kwa hekima na kwa Roho. Lakini viongozi wa sinagogi hawakupenda kile alichokuwa akifundisha. Walisema alikuwa anazungumza kinyume na Musa na kinyume na Mungu. Walimleta Stefano mbele ya kuhani mkuu na viongozi wengine.
Matendo ya Mitume 6: 9–15; 7:1
Uso wa Stefano ulionekana kama uso wa malaika. Aliwakumbusha viongozi kwamba Mungu alimtuma Musa kuwaokoa Waisraeli, lakini daima hawakumfuata Musa. Stefano alisema kwamba Musa alikuwa kama Yesu Kristo. Mungu alimtuma Yesu ili awaokoe watu Wake, lakini viongozi hawakumfuata. Viongozi walimkasirikia Stefano.
Matendo ya Mitume 7:20–43, 51–54
Akiwa amejawa Roho Mtakatifu, Stefano alitazama mbinguni. Alimwona Yesu Kristo akiwa amesimama kando ya Baba wa Mbinguni.
Matendo ya Mitume 7:55–56
Stefano alipowaambia viongozi kile alichokiona, walikasirika zaidi. Walipiga kelele kwa hasira na kumshika Stefano. Kisha walimburuza na kumtoa nje ya mji.
Matendo ya Mitume 7:57
Waliweka nguo zao miguuni pa mtu aliyeitwa Sauli. Kisha wakamrushia mawe Stefano ili kumuua. Sauli alikubaliana na kile walichokuwa wakifanya. Stefano alisali. Alimwomba Bwana awasamehe watu waliokuwa wakimuumiza. Pia alimwomba Bwana aipokee roho yake mbinguni.
Matendo ya Mitume 7:59–60; 8:1