Luka 7:36–50
Yesu Anamsamehe Mwanamke
“Alipenda sana”
Mtu aliyeitwa Simoni alimwalika Yesu aje nyumbani kwake na kula pamoja naye. Simoni alikuwa mmoja wa kundi la viongozi walioitwa Mafarisayo.
Luka 7:36
Walipokuwa wakila, mwanamke alikuja nyumbani kwa Simoni. Alikuwa amesikia kwamba Yesu alikuwa pale. Alitaka kuonyesha shukrani na upendo wake Kwake.
Luka 7:37
Mwanamke alilia alipomwona Yesu. Machozi yake yaliosha miguu Yake. Kisha akapangusa miguu Yake kwa nywele zake. Aliibusu miguu Yake na kuipaka mafuta yenye harufu nzuri.
Luka 7:38
Simoni alijua kwamba mwanamke huyu alikuwa ametenda dhambi nyingi. Alifikiria kwamba kama kweli Yesu alikuwa mtu wa Mungu, Yeye angejua kwamba mwanamke huyu alikuwa mwenye dhambi, na hangemruhusu kumgusa.
Luka 7:39
Yesu alijua kile Simoni alichokuwa anakifikiria. Yeye alimwambia Simoni kwamba yule mwanamke alikuwa ameosha miguu Yake kwa sababu alimpenda Yeye. Kwa kawaida, wageni walipewa maji ya kuosha miguu yao. Simoni hakuwa amefanya kitu chochote kama hicho ili kuonyesha upendo kwa Yesu.
Luka 7:40–47
Yesu alimwambia mwanamke yule kuwa alikuwa amesamehewa dhambi zake kwa sababu alimpenda na alikuwa na imani Kwake. Yeye alimwambia angeweza kwenda kwa amani.
Luka 7:47–50