Hadithi za Maandiko
Yesu na Kijana Tajiri—"Nifanye nini nipate kuurithi uzima wa milele?"


Marko 10:17–31

Yesu na Kijana Tajiri

"Nifanye nini nipate kuurithi uzima wa milele?"

Mvulana akimkimbilia Yesu.

Wakati Yesu na wanafunzi Wake walipokuwa wakisafiri, kijana tajiri alikuja akimkimbilia Yesu na kupiga magoti mbele Yake. Alimuuliza Yesu kile anachopaswa kufanya ili kuishi na Baba wa Mbinguni tena.

Marko 10:17

Yesu anamkumbusha mvulana huyo kuhusu amri.

Mwokozi alimkumbusha kijana kwamba tayari alijua amri za Mungu: usiue, usidanganye au kuiba, na kumheshimu baba na mama yako.

Marko 10:19

Kijana anamjibu Yesu.

Mvulana huyo alijibu kwamba daima alikuwa ametii amri hizi, tangu alipokuwa mtoto.

Marko 10:20

Yesu anamfundisha kijana.

Yesu alimtazama yule mvulana kwa upendo. Yeye alimwambia kwamba alihitaji kufanya kitu kimoja zaidi. Yeye alihitaji kuuza kila kitu alichokuwanacho, kuwapa maskini pesa, na kuwa mmoja wa wafuasi wa Yesu. Kisha angekuwa na hazina mbinguni!

Marko 10:21

Yule mvulana anaondoka.

Yule mvulana alikuwa tajiri sana. Hakutaka kutoa kila kitu alichokuwanacho. Aliondoka akihisi huzuni.

Marko 10:22

Yesu anaelezea kwamba tunapaswa kumtumainia Mungu, si utajiri.

Yesu alisema ni rahisi zaidi kwa ngamia kupitia tundu la sindano kuliko ilivyo kwa watu wanaopenda utajiri kuingia katika ufalme wa Mungu. Wanafunzi walishangaa. "Ni nani, basi, awezaye kuokoka ?" waliuliza. Yesu alielezea kwamba tunapaswa kumtumainia Mungu ili tuokolewe. "Maana yote yawezekana kwa Mungu," Yeye alisema.

Marko 10:23–30