Hadithi za Maandiko
Mfano wa Msamaria Mwema—Kuwapenda majirani zetu kama tunavyojipenda wenyewe


Luka 10:25–37

Mfano wa Msamaria Mwema.

Kuwapenda majirani zetu tunavyojipenda wenyewe

Mtu anamwuliza Yesu swali.

Mwanasheria alimwuliza Yesu jinsi ya kupokea uzima wa milele. Yesu alimuuliza kile kilichoandikwa katika maandiko. Mwanasheria alijibu kwamba maandiko yanasema kumpenda Mungu na kumpenda jirani yetu. Yesu alisema alikuwa sahihi. Kisha mwanasheria aliuliza, “Na jirani yangu ni nani?” Yesu alijibu kwa kumwambia mfano au hadithi.

Luka 10:25–29

Mtu Myahudi amejeruhiwa na wezi.

Katika mfano, mtu ambaye alikuwa Myahudi alikuwa akisafiri barabarani kutoka Yerusalemu hadi Yeriko. Ghafla, wezi wakaja. Walimwibia nguo zake, wakamjeruhi vibaya, na wakamwacha pale.

Luka 10:30

Kuhani anampuuza yule mtu aliyejeruhiwa.

Punde, kuhani akashuka barabarani. Kuhani huyu alikuwa mtu aliyefanya kazi hekaluni. Alimwona mtu yule barabarani lakini akapita upande mwingine.

Luka 10:31

Mlawi anampuuza mtu aliyejeruhiwa.

Kisha akaja mtu mwingine ambaye pia alifanya kazi hekaluni, aliyeitwa Mlawi. Alimwona mtu yule aliyejeruhiwa, lakini alipita upande mwingine wa barabara pia.

Luka 10:32

Msamaria anamwona mtu Myahudi.

Kisha Msamaria alitembea karibu. Aliona kwamba mtu yule barabarani alijjeruhiwa vibaya sana. Wasamaria na Wayahudi kwa kawaida hawakuwa na uhusiano mzuri. Lakini Msamaria huyu alitaka kumsaidia mtu yule.

Luka 10:33

Msamaria anamshughulikia mtu Myahudi.

Msamaria alimshughulikia mtu huyo kwa kumweka mafuta na divai kwenye majeraha ya mtu huyo. Alimpandisha mtu yule juu ya punda wake.

Luka 10:34

Msamaria anampeleka yule Myahudi kwenye nyumba ya wageni.

Kisha Msamaria alimleta mtu yule kwenye nyumba ya wageni, ambapo angeweza kupumzika na kupata nafuu. Kabla ya Msamaria kuondoka siku iliyofuata, alimpa mwenye nyumba ya wageni pesa na kusema, “Mtunze huyu.” Msamaria alisema angerudi baada ya siku chache na pesa zaidi.

Luka 10:34–35

Yesu anamwambia mwanasheria awe kama yule Msamaria.

Mwishoni mwa hadithi, Yesu alimuuliza mwanasheria swali. Ni nani aliyekuwa jirani wa yule mtu aliyejeruhiwa? Kuhani, Mlawi, au Msamaria? Mwanasheria alisema ni yule aliyeonyesha upendo kwa mtu yule—Msamaria. Yesu alimwambia mwanasheria aende na kuwa kama Msamaria.

Luka 10:36–37