2 Wakorintho 12:7–10
Yesu Kristo anaweza kufanya vitu dhaifu kuwa Vyenye Nguvu.
Somo la Paulo kutoka kwenye “mwiba”
Mtume Paulo alikuwa mtumishi hodari wa Yesu Kristo. Alikuwa na mafunuo mengi na kuwafundisha watu kuhusu Mwokozi. Lakini Paulo pia alikuwa na changamoto nyingi.
2 Wakorintho 12:7
Katika barua kwa waumini wa Kanisa, Paulo alilinganisha changamoto zake na kuwa na mwiba uliokwama kwenye ngozi yake. Ulimfanya Paulo kujisikia dhaifu sana.
2 Wakorintho 12:7
Mara tatu, Paulo alisali na kumwomba Bwana aondoe changamoto yake. Lakini Bwana hakuiondoa.
2 Wakorintho 12:8–9
Badala yake, Bwana alimwambia Paulo kwamba alikuwa na uwezo wa kutosha kumfanya Paulo kuwa na nguvu. Paulo alijifunza kwamba wakati mwingine changamoto inaweza kuwa kitu kizuri ikiwa tutamgeukia Bwana na kuomba msaada. Tunapojisikia kuwa wadhaifu, Yesu Kristo anaweza kutufanya kuwa imara, hata kama changamoto zetu haziondoki.
2 Wakorintho 12:9–10