Luka 15
Kondoo Aliyepotea, Sarafu Iliyopotea, na Mwana Aliyepotea
Mifano mitatu kuhusu upendo wa Mungu
Baadhi ya viongozi wa Kiyahudi walimwona Yesu akizungumza na kula pamoja na watu ambao walidhani walikuwa wenye dhambi. Viongozi walidhani ni makosa kwa Yesu kula pamoja na wenye dhambi. Yesu aliwaambia viongozi wale hadithi tatu au mifano ili kuwasaidia kuelewa kwamba Yeye anataka kumsaidia kila mtu kutubu na jinsi Yeye alivyo na furaha wakati wanapofanya hivyo.
Luka 15:1–3
Mfano wa kwanza ulikuwa kuhusu mtu aliyekuwa na kondoo 100. Mmoja wa kondoo wake alipotea.
Luka 15:4
Mtu yule aliwaacha kondoo wengine 99 na kwenda kumtafuta yule aliyepotea. Aliendelea kumtafuta mpaka akampata.
Luka 15:4
Hatimaye alipompata kondoo wake aliyepotea, alikuwa na furaha sana! Alimbeba kondoo nyumbani mabegani mwake na kuwaambia rafiki zake na majirani wafurahi pamoja naye. Yesu alisema hivi ndivyo Baba wa Mbinguni anavyojisikia wakati mtu anapotubu dhambi zake na kurudi Kwake.
Luka 15:5–7
Mfano wa pili ulikuwa kuhusu mwanamke aliyekuwa na sarafu 10 za fedha. Alipopoteza moja, aliwasha mshumaa na kufagia nyumba yake, akitafuta sarafu iliyopotea. Aliendelea kutafuta mpaka akaipata.
Luka 15:8
Hatimaye alipopata sarafu iliyopotea, alikuwa na furaha sana! Aliwaambia rafiki zake na majirani zake wafurahi pamoja naye. Yesu alisema hivi ndivyo malaika wa mbinguni wanavyojisikia wakati mtu anapotubu dhambi zake.
Luka 15:9–10
Mfano wa tatu ulikuwa juu ya mtu aliyekuwa na wana wawili. Mwana mdogo hakutaka kuishi tena na baba yake. Alimwomba baba yake kumpa sehemu yake ya pesa za familia sasa. Kisha mwana yule akaondoka nyumbani na kwenda kwenye nchi mbali sana.
Luka 15:11–13
Mwana alifanya chaguzi mbaya sana. Alitumia vibaya pesa ambazo baba yake alikuwa amempa yeye.
Luka15:13
Baada ya pesa zake zote kuwa zimeisha, alikuwa na njaa sana. Hakuna mtu ye yote ambaye angempa kitu cho chote cha kula. Hatimaye alipata kazi ya kuwalisha nguruwe. Mwana yule alikuwa na njaa sana, alitamani angekula chakula cha nguruwe. Alijua alihitaji kurudi kwa baba yake.
Luka 15:14–18
Lakini mwana huyo hakuwa na uhakika kama baba yake angemkaribisha tena. Aliamua angemuomba baba yake kama angeweza kuwa mmoja wa watumishi wake.
Luka 15:17–19
Mwana alipokuwa akitembea kwenda nyumbani, baba yake alimwona akija kwa mbali sana. Baba alikuwa na furaha sana, alimkimbilia mwanawe!
Luka 15:20
Baba alimkumbatia mwanawe na kumbusu. Aliwaambia watumishi wake walete nguo nzuri zaidi kwa ajili ya mwanawe na kuandaa karamu. Alitaka kila mtu kusherehekea na kuwa na furaha kwa sababu mwanawe alikuwa amerudi nyumbani.
Luka 15:20–24
Wakati huu wote, mwana mkubwa alikuwa akifanya kazi shambani. Aliporudi nyumbani, alisikia muziki na dansi. Alimuuliza mtumishi kile kilichokuwa kinaendelea. Mtumishi alimwambia kwamba kaka yake mdogo alikuwa amerudi nyumbani, hivyo walikuwa na karamu ya kusherehekea.
Luka 15:25–27
Kaka mkubwa alikasirika. Baba yake alimwalika kwenye karamu, lakini hakwenda. Alimwambia baba yake kwamba yeye alikuwa amemtumikia kwa miaka mingi, lakini hakuna mtu aliyewahi kumfanyia karamu. Baba alimwambia, “Yote niliyonayo ni yako,” lakini ilikuwa vizuri kuwa na furaha wakati mtu anapotubu na kurudi nyumbani!
Luka 15:28–32