Luka 24:1–12, 36–49; Yohana 20
Amefufuka
Yesu Kristo anashinda mauti kwa ajili ya wote
Wanafunzi wa Yesu waliuweka mwili Wake kaburini. Walitaka kufanya zaidi kuutunza mwili Wake, lakini ilikuwa karibu Sabato. Walipanga kurudi baada ya Sabato kumaliza.
Luka 23:52–56
Mapema asubuhi siku ya tatu baada ya kifo cha Yesu, Mariamu Magdalena na wengine walikwenda kaburini.
Luka 24:1; Yohana 20:1
Walipofika, waliona kwamba jiwe lililofunika kaburi lilikuwa limevingirishwa mbali. Walikwenda kaburini, na mwili wa Yesu haukuwepo.
Luka 24:2–3; Yohana 20:1
Mariamu alikimbia kuwaambia Petro na Yohana kwamba mtu alikuwa ameuchukua mwili wa Yesu. Petro na Yohana walikimbilia kaburini.
Yohana 20:2–4
Walipofika kaburini, Petro na Yohana waliingia ndani. Waliona kwamba mwili wa Yesu ulikuwa haupo. Kitambaa ambacho Yeye alikuwa amefunikwa nacho bado kilikuwa pale.
Yohana 20:5–7
Petro na Yohana walienda nyumbani, lakini Mariamu alikaa kaburini, akilia. Alitazama kaburini na kuona malaika wawili. Walimwuliza kwa nini alikuwa akilia. Alisema mtu alikuwa ameuchukua mwili wa Yesu, na hakujua pale ulipo.
Yohana 20:11–13
Kisha Yesu akaja, lakini Mariamu hakujua ilikuwa ni Yeye. Yesu alimwuliza, "Mama, unalilia nini?" Mariamu alifikiri Yeye alikuwa mtunza bustani. Alimuuliza kama alijua pale mwili wa Yesu ulipokuwa.
Yohana 20:14–15
Yesu alisema, "Mariamu." Mariamu aligeuka. Sasa alijua kwamba alikuwa ni Yesu! Mariamu alisema Kwake, "Bwana." Yesu alimwomba awaambie wanafunzi wengine kwamba Yeye alihitaji kwenda kwa Baba Yake wa Mbinguni. Mariamu aliwapata wanafunzi wengine na kuwaambia kwamba alikuwa amemwona Yesu na Yeye alikuwa hai tena!
Yohana 20:16–18
Jioni ile, wengi wa Mitume walikuwa pamoja. Walifunga milango, wakiogopa kwamba viongozi wa Wayahudi wangejaribu kuwatafuta. Ghafla, walimwona Yesu akiwa amesimama miongoni mwao. Mwanzoni waliogopa. Walidhani Yeye alikuwa ni roho. Yesu alisema, "Amani iwe kwenu."
Luka 24:33–38; Yohana 20:19
Yesu aliwaalika Mitume kugusa mikono na miguu Yake. Yeye aliwataka wajue kwamba Yeye alikuwa na mwili, sio tu roho. Hata alikula samaki na asali pamoja nao. Wanafunzi walikuwa na furaha sana kumwona Yeye!
Luka 24:39–44; Yohana 20:20
Kisha Yesu aliwasaidia Mitume Wake kuelewa maandiko ambayo yalifundisha kuhusu kifo Chake na Ufufuko Wake. Yeye aliwataka wamfundishe kila mtu kwamba kwa sababu Yake, wangeweza kutubu na kusamehewa. Mitume wangekuwa mashahidi Wake.
Luka 24:44–48
Mtume Tomaso hakuwepo wakati Yesu alipokuja. Alisema asingeamini kwamba Yesu alikuwa hai isipokuwa aweze kuona alama za misumari mikononi Mwake.
Yohana 20:24–25
Siku nane baadaye, wanafunzi walikusanyika pamoja. Yesu alitokea tena. Wakati huu Tomaso alikuwa pale.
Yohana 20:26
Yesu alimwalika Tomaso kugusa majeraha katika mikono yake na ubavuni Mwake. Yeye alimwambia Tomaso, "Wala usiwe asiyeamini, bali aaminiye." Tomaso alisema, "Bwana wangu na Mungu wangu." Sasa Tomaso aliamini kwamba Yesu alifufuka. Yesu alisema kwamba watu wanabarikiwa wanapoamini, hata kama hawajamwona Yeye.
Yohana 20:27–29