Luka 4:16–31
Yesu Anashuhudia Juu ya Misheni Yake
Anakataliwa huko Nazareti
Yesu alikwenda Nazareti, ambapo familia yake na marafiki waliishi. Palikuwa mahali ambapo Yeye alikulia. Siku ya Sabato, alienda kwenye sinagogi, ambapo watu walikwenda kujifunza maandiko na kumwabudu Mungu.
Luka 4:16–17
Katika sinagogi, Yesu alisimama na kusoma maandiko kutoka kwa nabii Isaya. Maandiko yalisema kwamba siku moja Mwokozi angekuja. Yeye angehubiri injili kwa masikini na kuponya mioyo iliyovunjika. Yeye angewasaidia vipofu na wale walioumia.
Isaya 61:1–2; Luka 4:17–19
Yesu alimaliza kusoma na kukaa chini. Kila mmoja alikuwa akimtamaza Yeye. Yeye aliwaambia kwamba katika siku ile hasa, maandiko aliyoyasoma yalikuwa yanatimia. Yeye alikuwa Mwokozi.
Luka 4:21
Watu wa Nazareti walishangazwa sana na kile Yesu alichokisema. Ni kwa jinsi gani Yesu angeweza kuwa Mwokozi? Walidhani Yeye alikuwa tu mwana wa Mariamu na Yusufu, si Mwana wa Mungu. Kwao, Yeye alionekana kama mtu wa kawaida.
Luka 4:22
Yesu alijua kwamba watu walimtaka Yeye afanye muujiza ili kuthibitisha kwamba Yeye alikuwa Mwokozi. Alifundisha kwamba miujiza ilikuwa kwa watu ambao wanaamini, na wakati mwingine Mungu alifanya miujiza kwa wale ambao hawakuwa wa Israeli kwa sababu walikuwa na imani zaidi. Baadhi ya watu katika sinagogi walimkasirikia Yesu.
Luka 4:23–28
Walimlazimisha Yeye kuondoka mjini na kupanda hadi juu ya kilima. Walitaka kumtupa kutoka kilimani.
Luka 4:28–29
Lakini Yesu alipita katikati ya watu wenye hasira.
Luka 4:30
Kwa sababu hawakumtaka Yeye katika Nazareti, Yesu alienda mji mwingine kufundisha.
Luka 4:31–32