Matthayo 14:13–21; Yohana 6
Yesu Anawalisha Maelfu ya Watu
Yeye ni Mkate wa Uzima.
Yesu aligundua kwamba Yohana Mbatizaji alikuwa ameuawa. Yeye alikwenda mahali mbali sana na miji ili aweze kuwa na muda peke yake.
Mathayo 14:13
Wakati watu waliposikia pale Yesu alipokuwa ameenda, walimfuata. Yesu aliwaona, na Yeye alihisi upendo kwa ajili yao. Alitumia siku nzima kuwabariki na kuwaponya.
Mathayo 14:13–14
Karibu na mwisho wa siku, watu walikuwa wanasikia njaa. Mitume walidhani Yesu alipaswa kuwarudisha watu kwenye miji ili wakapate chakula. Lakini Yesu aliwataka wabakie. Yeye aliwaomba Mitume kuwapa watu kitu cha kula.
Mathayo 14:15–16
Mtume Andrea alimpata mvulana aliyekuwa na mikate mitano na samaki wawili wadogo ili kuwapa watu. Lakini kulikuwa na wanaume 5,000, pamoja na wanawake na watoto, ambao walihitaji kula. Ni kwa jinsi gani wangeweza kuwalisha watu wengi sana kwa chakula kidogo kama kile?
Mathayo 14:17, 21; Yohana 6:8–10
Yesu aliwaomba Mitume kuleta chakula Kwake. Yeye aliwaambia watu waketi chini. Kisha Yesu akasema sala ya kumshukuru Baba wa Mbinguni kwa ajili ya mkate na samaki na kuvibariki. Kisha akamega mkate na samaki vipande vipande.
Mathayo 14:18–19; Yohana 6:10–11
Yesu aliwaomba Mitume Wake wawape watu mkate na samaki. Kila mtu alikula, na kila mtu alikuwa ameshiba. Baada ya kula, bado kulikuwa na vikapu 12 vilivyojaa chakula cha mabaki!
Mathayo 14:20; Yohana 6:11–13
Siku iliyofuata, watu walirudi na kumpata Yesu tena. Lakini Yesu alijua kwamba wengi wao walikuwa wanamfuata Yeye kwa sababu tu alikuwa amewapa chakula. Yesu aliwakumbusha kwamba chakula hudumu kwa muda mfupi tu. Yeye alikuwa na kitu bora cha kuwapa.
Yohana 6:14, 24–27
Yesu alisema, “Mimi ndimi mkate wa uzima.” Mkate hutupatia uhai duniani. Lakini Yesu Kristo anaweza kutupatia uzima wa milele pamoja na Baba wa Mbinguni.
Yohana 6:35–58
Watu wengi hawakupenda kile Yesu alichokuwa anajaribu kufundisha. Waliondoka na kuamua kutomfuata Yesu tena.
Yohana 6:60, 66
Kisha Yesu akawaambia Mitume Wake, “Je, ninyi nanyi mwataka kuondoka?” Petro alijibu, “Bwana, twende kwa nani? Wewe unayo maneno ya uzima wa milele.” Mitume hawakuaondoka. Walijua kwamba Yesu Kristo alikuwa Mwokozi na Mwana wa Mungu.
Yohana 6:67–69