Luka 2:39–52
Mvulana Yesu
Kujifunza na kukua
Yesu alikulia katika mji wa Nazareti akiwa na Mariamu na Yusufu. Baada ya muda, Yeye alijifunza zaidi na zaidi kuhusu Baba wa Mbinguni. Yeye alijiandaa kwa ajili ya kazi ambayo Baba wa Mbinguni alimtaka Yeye aifanye.
Luka 2:39–40; Mafundisho na Maagano 93: 12–14
Wakati Yesu alipokuwa na umri wa miaka 12, alikwenda Yerusalemu pamoja na familia na marafiki kusherehekea Pasaka. Walikaa huko kwa siku kadhaa.
Luka 2:41–43
Walipokuwa wanarudi nyumbani, Mariamu na Yusufu waligundua kwamba Yesu hakuwa pamoja nao. Walirudi Yerusalemu kumtafuta. Walikuwa na wasiwasi sana.
Luka 2:44–46
Baada ya kutafuta kwa siku tatu, Mariamu na Yusufu hatimaye walimpata Yesu. Yeye alikuwa hekaluni, akizungumza na baadhi ya walimu kuhusu maandiko. Walimu walikuwa wakimwuliza Yeye maswali. Walishangazwa na jinsi Yesu alivyojua na kuelewa!
Luka 2:46–47; ona pia Tafsiri ya Joseph Smith katika tanbihi 46c
Mariamu alimwambia Yesu jinsi walivyokuwa na wasiwasi wakati ambapo hawangeweza kumpata Yeye. Yesu alijibu kwamba Yeye alikuwa akifanya kazi ya Baba Yake. Yesu alirudi Nazareti pamoja na familia Yake. Yeye alimtii Mariamu na Yusufu.
Luka 2:48–52
Yesu aliendelea kujifunza. Alikuwa mkubwa na mwenye nguvu zaidi. Baba wa Mbinguni alimpenda Yeye na alimsaidia Yeye kujiandaa kwa ajili ya misheni Yake. Yesu aliwapenda watu waliomzunguka, na wao walimpenda Yeye.
Luka 2:52