Mathayo 1; Luka 1
Malaika Wanamtembelea Mariamu na Yusufu
Wateule wa kumtunza Mwana wa Mungu
Mwanamke aliyeitwa Mariamu aliishi katika mji wa Nazareti. Alimpenda Mungu na kutii amri Zake. Mariamu alikuwa anatarajia kuolewa na mtu aitwaye Yusufu, ambaye pia alimpenda Mungu.
Mathayo 1:18–19; Luka 1:26–28
Siku moja malaika aliyeitwa Gabrieli alimtembela Mariamu. Mwanzoni, Mariamu aliogopa. Lakini Gabrieli alisema kwamba alitumwa kutoka kwa Mungu. Mariamu hakupaswa kuogopa. Alisema kwamba Mariamu alikuwa maalum sana kwa Mungu na punde angepata mtoto. Mtoto wa Mariamu angekuwa Mwana wa Mungu, Yesu.
Luka 1:26–33
Lakini Mariamu alikanganyikiwa. Hakuwa bado ameolewa na Yusufu. Angewezaje kupata mtoto? Gabrieli alieleza kwamba itatokea kupitia nguvu za Mungu. Alimwambia “kwa Mungu hakuna lisilowezekana.”
Luka 1:34–37
Mariamu alikuwa mnyenyekevu na mwaminifu. Alimwambia Gabrieli kwamba alikuwa mtumishi wa Bwana. Alikuwa tayari kuwa mama wa Mwana wa Mungu.
Luka 1:38
Wakati Yusufu alipogundua kwamba Mariamu atapata mtoto, alifadhaika. Alijiuliza ikiwa bado angepaswa kumuoa Mariamu.
Mathayo 1:19
Lakini usiku mmoja katika ndoto, malaika alimtembelea Yusufu. Malaika alimwambia Yusufu kwamba mtoto wa Mariamu alikuwa Mwana wa Mungu na Yusufu anapaswa kumwita Yeye Yesu. Yesu angewaokoa watu wote kutokana na dhambi zao. Malaika alisema Yusufu bado alipaswa kumuoa Mariamu.
Mathayo 1:20–23
Yusufu alifanya kile malaika alichosema. Yusufu na Mariamu walioana.
Mathayo 1:24
Mariamu alikwenda kumtembelea Elisabeti, binamu yake. Malaika alimwambia Mariamu kwamba Elisabeti pia alikuwa mjamzito, ingawa alikuwa mzee sana. Huu ulikuwa muujiza mwingine kutoka kwa Mungu. Mwanaye angekua na kuwa Yohana Mbatizaji. Wakati Mariamu alipoingia ndani ya nyumba, alimsalimu Elisabeti.
Luka 1:13–17, 36, 39–40
Punde tu Elisabeti alipomsikia Mariamu, mtoto wa Elisabeti aliruka kwa furaha ndani ya tumbo lake. Elisabeti alijawa na Roho Mtakatifu. Alijua Mariamu alikuwa na ujauzito wa Mwana wa Mungu. Mariamu alifurahia pamoja na Elisabeti. Alimsifu Mungu kwa mambo yote mazuri Yeye anayofanya kuwabariki watoto Wake.
Luka 1:41–55