Yohana 11:1–46
Yesu Anamfufua Lazaro
“Mimi ndimi huo ufufuko, na uzima”
Mariamu, Martha, na Lazaro waliishi katika mji ulioitwa Bethania. Walimwamini Yesu, na Yeye aliwapenda. Mariamu na Martha walikuwa madada wa Lazaro.
Yohana 11:1, 5
Lazaro akawa mgonjwa sana. Yesu alikuwa katika mji mwingine. Mariamu na Martha walimtumia Yeye ujumbe kumjulisha kuwa rafiki Yake alikuwa mgonjwa.
Yohana 11:1–3
Yesu alisubiri kwa siku mbili. Kisha Yeye akawaambia wanafunzi Wake kwamba wangeenda Bethania. Wanafunzi walikuwa na wasiwasi kwa sababu baadhi ya watu waliokuwa karibu na Bethania walitaka kumuumiza Yesu. Lakini Yesu alitaka kumsaidia Lazaro. Yesu alisema kwamba Lazaro alikuwa tayari amekwisha kufa, na Yeye alikuwa anaenda kumfufua.
Yohana 11:6–16
Martha alimlaki Yesu nje ya mji. Alisema kwamba kama Yesu angekuja mapema, Lazaro hangekufa. Yesu aliahidi kwamba Lazaro angeishi tena.
Yohana 11:17–24
Yesu alisema, “Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima.” Yeye alimuuliza Martha kama alimwamini Yeye. Alisema, “Ninaamini kwamba wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu.”
Yohana 11:25–27
Martha alirudi nyumbani na kumwambia Mariamu kwamba Yesu alikuwa amekuja. Mariamu alikuja na kuanguka miguuni pa Yesu, akilia kumhusu kaka yake. Yesu alilia pia. Yeye aliwapenda Lazaro, Mariamu, na Martha.
Yohana 11:28–36
Yesu, Martha, Mariamu, na wengine walienda kwenye pango mahali ambapo Lazaro alizikwa. Jiwe kubwa lilifunika lango. Yesu alisema liondoeni jiwe.
Yohana 11:38–39
Lakini Martha alimwambia Yesu kwamba Lazaro alikuwa tayari amekufa siku nne. Yesu alimkumbusha Martha kuhusu ahadi Yake. Yeye alimwomba aamini.
Yohana 11:39–40
Kisha Yesu akaomba kwa Baba Yake. Yeye alimshukuru Mungu kwamba daima amekuwa akimsikiliza Yeye. Yesu alitaka watu waamini kwamba Mungu alikuwa amemtuma Yeye kuwa Mwokozi. Kisha Yesu akaita, “Lazaro, njoo nje.”
Yohana 11:41–43
Lazaro alitoka nje ya lile pango. Bado alikuwa amefunikwa na nguo na shuka alizokuwa amezikwa nazo. Yesu aliwaambia watu wamfungue. Watu wengi waliokuwa wakitazama siku hiyo sasa waliamini kwamba Yesu kweli alikuwa Mwokozi, Mwana wa Mungu.
Yohana 11:44–45