Mathayo 16–17
Yesu Anawapa Mitume Wake Funguo za Ukuhani
“Juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu”
Siku moja, Yesu aliwauliza wanafunzi Wake watu walidhani Yeye alikuwa ni nani. Wanafunzi Wake walijibu kwamba baadhi ya watu walisema Yeye alikuwa Yohana Mbatizaji. Wengine walidhani Yeye alikuwa nabii kutoka Agano la Kale ambaye alikuwa amerudi.
Mathayo 16:13–14
Kisha Yesu aliwauliza wanafunzi Wake walidhani Yeye alikuwa ni nani. Petro alisema, “Wewe ndiye Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai.”
Mathayo 16:15–16
Yesu alifurahi kumsikia Petro akisema hivi. Alimwambia Petro kwamba hakujua Yesu alikuwa nani kutoka kwa watu wengine. Baba wa Mbinguni alimfunulia hilo.
Mathayo 16:17
Yesu alimwambia Petro, “Juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu.” Kisha Yeye aliahidi kumpa Petro funguo za ukuhani, au mamlaka kutoka kwa Mungu, hivyo yeye na Mitume wengine wangeweza kuliongoza Kanisa Lake duniani.
Mathayo 16:18–19
Siku chache baadaye, Yesu alimchukua Petro, Yakobo, na Yohana juu ya mlima mrefu ili kusali.
Mathayo 17:1; Luka 9:28
Wakati Yesu akisali, uso Wake uling’aa kama jua. Hata nguo Zake zilionekana angavu.
Mathayo 17:2; Luka 9:29
Manabii wawili kutoka Agano la Kale, Musa na Eliya, walitokea. Walizungumza na Yesu kuhusu kifo Chake na Ufufuo, ambavyo vingetokea hivi karibuni katika Yerusalemu. Petro alimwambia Yesu, “Bwana, ni vizuri sisi kuwapo hapa.”
Mathayo 17:3–4; Luka 9:30–33 (ona Tafsiri ya Joseph Smith katika tanbihi 31a)
Wakati Petro alipokuwa akiongea, wingu angavu liliwazingira. Walisikia sauti ya Baba wa Mbinguni ikishuhudia, “Huyu ni Mwanangu, mpendwa, ninayependezwa Naye, msikilizeni yeye.” Petro, Yakobo, na Yohana waliogopa na wakaanguka chini.
Mathayo 17:5–6
Yesu aliwagusa Mitume Wake na kusema, “Inukeni, wala msiogope.” Walitazama juu. Musa na Eliya walikuwa wameondoka. Juu ya mlima huu, Petro, Yakobo, na Yohana walipokea funguo za ukuhani ambazo Yesu alikuwa amewaahidi.
Mathayo 17:7–9; ona pia Mafundisho na Maagano 27:12–13