“ ‘Udhibiti Mkali’ huko Ghana,” Hadithi za Mafundisho na Maagano (2024)
“ ‘Udhibiti Mkali’ huko Ghana,” Hadithi za Mafundisho na Maagano
Juni 1989–Novemba 1990
“Udhibiti Mkali” huko Ghana
Kubaki mwaminifu wakati Watakatifu hawawezi kukusanyika
Alice Johnson alikuwa mmisionari anayehudumu katika nchi yake ya nyumbani, Ghana. Alipenda kushiriki ushuhuda wake juu ya Yesu Kristo na kusaidia Kanisa kukua.
Saints, 4:416–17
Siku moja, Alice alipata habari za kukasirisha. Serikali huko Ghana ilikuwa imesema hakungekuwa tena na mikutano ya Kanisa. Wamisionari hawangeweza tena kufundisha.
Saints, 4:417
Maafisa wa polisi waliwafanya wamisionari kuondoka kwenye nyumba zao na kuchukua baiskeli zao. Baadhi ya waumini wa Kanisa waliwekwa jela. Askari walifunga majengo ya Kanisa na hawangemruhusu mtu yeyote kuingia ndani yake. Watu waliita hii “uthibiti mkali.”
Saints, 4:417–18
Wamisionari iliwabidi waende nyumbani. Alice alikwenda kuishi na rafiki katika mji mwingine. Alikuwa na wasiwasi kwamba kamwe hangeweza kumaliza misheni yake.
Saints, 4:418
Watakatifu huko Ghana walichanganyikiwa, walihuzunika, na waliogopa. Walijiuliza ni kitu gani walichokosea. Je, wangeweza kwenda tena kanisani?
Saints, 4:418
Japokuwa hawakuweza kukusanyika pamoja na kata zao, Watakatifu bado walimpenda Bwana na walitaka kumwabudu Yeye. Walikuwa na mikutano ya sakramenti majumbani mwao. Wanafamilia ambao walikuwa na ukuhani walibariki mkate na maji na kuupitisha kwa familia yote.
Mafundisho na Maagano 6:32; Saints, 4:419
Mwezi baada ya mwezi, uthibiti mkali uliendelea. Watakatifu waliimba nyimbo na kufundishana injili majumbani mwao. Walitembeleana kusaidia kubakiza imani yao kuwa imara. Waliweka kando zaka yao ili kulipa wakati ambapo wangeweza kurudi kanisani. Walisali na kufunga ili uthibiti huo mkali uishe
Saints, 4:436–37
Hatimaye, baada ya miezi 18, serikali iliamua kwamba Kanisa lingeweza kufanya mikutano tena. Rais mpya wa misheni aliomba kuzungumza na Alice, ambaye sasa alikuwa mwanafunzi chuoni. “Je, ungependa kurudi na kuhudumu misheni baada ya shule?” alimwuliza. “Hapana,” yeye alisema. “Ninataka kuhudumu sasa hivi!”
Saints, 4:437–39
Alice na Watakatifu wengine walikuwa na furaha sana kwamba waliweza kwenda kanisani tena! Jumapili ya kwanza baada ya uthibiti mkali, mkutano wa sakramenti ulidumu kwa saa mbili kwa sababu watu wengi walitaka kutoa shuhuda zao. Walielezana jinsi Bwana alivyowabariki na kuwasaidia kubakiza imani yao kuwa imara.
Mafundisho na Maagano 20:75; Saints, 4:438