“Jela ya Liberty,” Hadithi za Mafundisho na Maagano (2024)
“Jela ya Liberty,” Hadithi za Mafundisho na Maagano
Oktoba 1838–Machi 1839
Jela ya Liberty
Kumpata Bwana wakati wa nyakati ngumu
Watu wengi walioishi Missouri hawakuwapenda Watakatifu. Gavana aliwatuma askari ili kuwafanya waondoke. Askari waliwafukuza Watakatifu kutoka majumbani mwao, waliiba vitu kutoka kwenye nyumba zao, na kuwajeruhi wengi wao.
Saints, 1:355–56, 362, 364
Askari waliwakamata Nabii Joseph Smith na viongozi wengine wa Kanisa.
Saints, 1:357–58
Joseph aliuliza kama angeweza kuwa na muda peke yake na familia yake. Askari walisema hapana. Walimchukua Joseph na wafungwa wengine.
Saints, 1:366
Usiku mmoja, Joseph na wafungwa wengine walisikiliza wakati walinzi wao wakicheka kuhusu mambo mabaya waliyokuwa wamewafanyia Watakatifu. Joseph hangeweza kuvumilia kusikia tena. Alisimama na kupiga kelele, “Nyamazeni!” Aliongea kwa nguvu za Mungu. Walinzi waliogopa. Walisema walisikitika na kuacha kuzungumza.
Saints, 1:367–68
Baadaye, Joseph na rafiki zake waliwekwa jela katika mji ulioitwa Liberty. Jela ilikuwa baridi sana, ndogo, na yenye giza. Walikuwa tu na majani machafu kulala. Kulikuwa na chakula kidogo tu, na kiliwafanya wagonjwa.
Saints, 1:369–70, 374, 384–85
Joseph alifikiria mengi kuhusu Watakatifu. Na aliwapenda wao. Alikuwa na wasiwasi juu yao. Lakini hakuweza kufanya chochote kuwasaidia.
Saints, 1:385–86
Joseph alisali sana. Alimuuliza Mungu alikuwa wapi na kwa nini hakuwasaidia Watakatifu. Je, Mungu alikuwa amesahau kumhusu yeye na Kanisa?
Mungu alijibu sala ya Joseph. Yeye alisema, “Mwanangu, amani iwe katika nafsi yako.” Yeye alimwambia Joseph kwamba changamoto zake hazitadumu milele, na zingekuwa kwa faida yake. Mungu alimkumbusha Joseph kwamba Yesu Kristo alikuwa amepitia hata mambo magumu zaidi. Yeye aliahidi kwamba angekuwa pamoja na Joseph “milele na milele.”