“Kambi ya Israeli,” Hadithi za Mafundisho na Maagano (2024)
“Kambi ya Israeli,” Hadithi za Mafundisho na Maagano
Novemba 1833–Februari 1835
Kambi ya Israeli
Kujifunza kumtumaini Bwana
Watakatifu ambao walikuwa wakiishi Independence, Missouri, walihitaji msaada. Walikuwa wamefanya kazi kwa bidii ili kujenga Sayuni kama Mungu alivyowaagiza. Lakini watu wengine katika mji hawakutaka wawe huko. Waliwafanya Watakatifu kukimbia makazi yao.
Saints, 1:195
Joseph Smith alikuwa anaishi Kirtland. Alisikia kuhusu kile kilichotokea kwa Watakatifu huko Missouri, na alikuwa na huzuni. Alisali ili kujua nini cha kufanya. Bwana alimwambia Joseph kutafuta watu wa kwenda pamoja naye huko Missouri. Walitumaini serikali ingewasaidia Watakatifu kurudishiwa nyumba zao.
Mafundisho na Maagano 103:1–2, 11–20, 30–34; Saints, 1:195–96
Takriban watu 100 walijitolea kujiunga naye. Nabii aliliita kundi hili Kambi ya Israeli. Walikuwa na shauku ya kwenda kuwasaidia Watakatifu huko Missouri.
Saints, 1:197–99
Brigham Young na rafiki yake Heber Kimball walikuwa sehemu ya kundi hilo. Mvulana aliyeitwa Wilford Woodruff alikuja kutoka umbali mrefu New York ili kusaidia.
Saints, 1:197–98
Watu zaidi walijiunga na kambi. Walitembea kwa mwezi mzima na kuvuka mto mpana kwenda Missouri. Walikuwa wamechoka na walikuwa na vidonda. Mwendo mrefu pia ulifanya baadhi ya watu kujisikia kukata tamaa. Bado walikuwa umbali mrefu kufika mji wa Independence.
Saints, 1:200–201
Walipokuwa wakiendelea kutembea, mwanamke aliwaita. Alisema kwamba baadhi ya watu walikuwa wanakuja kuwaua.
Saints, 1:203
Kambi ya Israeli ilisimama kwa usiku huo kwenye kilima juu ya mto. Walipopiga kambi, watu watano waliwajia wakiwa juu ya farasi. Walijivunia kwamba wanaume zaidi 300 walikuwa njiani kushambulia kambi hiyo. Washiriki wengi wa Kambi ya Israeli walikuwa na wasiwasi. Joseph aliwaambia wawe na imani kwamba Mungu angewasaidia.
Saints, 1:203
Punde anga lilijaa mawingu ya kijivu. Mvua kubwa ilianza kunyesha. Mto ulikuwa wa kina zaidi. Upepo uliangusha miti. Radi iliangaza angani. Joseph na wengine walipata kanisa dogo ambapo wangeweza kuwa salama. Waliimba nyimbo za dini usiku mzima. “Mungu yupo katika tufani hii!” Joseph alisema.
Saints, 1:203–4
Dhoruba ilikuwa imewazuia watu waliotaka kuwashambulia. Kambi ilikuwa salama. Lakini serikali ilisema haiwangewasaidia Watakatifu. Bwana alimwambia Joseph kwamba Kambi ya Israeli inaweza kwenda nyumbani. Watakatifu wanapaswa kujenga Sayuni kwa kutii amri za Mungu. Yeye aliahidi Ange “pigana vita vya Sayuni.”
Mafundisho na Maagano 105:1–19; Saints, 1:204–5
Baadhi ya washiriki wa kambi walikasirika waliposikia hili. Walihuzunika kwamba hawakupata kuipigania Sayuni. Baadhi ya watu walidhani Kambi ya Israeli ilikuwa imeshindwa. Lakini wengine, kama Brigham Young, Heber, na Wilford, walikuwa na shukrani kwa nafasi ya kuwa pamoja na Nabii Joseph na kujifunza kutoka Kwake.
Saints, 1:205–6
Baadaye, Bwana alimwambia Joseph Smith kuwaita Mitume Kumi na Wawili ili kusaidia kuongoza Kanisa Lake. Mitume wangekuwa mashahidi maalum wa jina la Yesu Kristo ulimwenguni kote. Wanane kati ya Mitume Kumi na Wawili walikuwa wametembea katika Kambi ya Israeli. Kuhudumu pamoja na Joseph kulisaidia kuwaandaa kwa ajili ya wito huu muhimu.
Mafundisho na Maagano 18:26–27; 107:23; Saints, 1:214–17