Hadithi za Maandiko
Newel na Ann Whitney Wanakutana na Nabii Joseph


“Newel na Ann Whitney Wanakutana na Nabii Joseph,” Hadithi za Mafundisho na Maagano (2024)

“Newel na Ann Whitney Wanakutana na Nabii Joseph,” Hadithi za Mafundisho na Maagano

Oktoba 1830–Februari 1831

Newel na Ann Whitney Wanakutana na Nabii Joseph

Sala za imani zilizojibiwa na Bwana

Ann na Newel Whitney wakisali.

Ann na Newel Whitney walimiliki duka huko Kirtland, Ohio. Ann hakukua akienda kanisani au kujifunza kuhusu Bwana, lakini alitaka kumjua Yeye. Baada ya yeye na Newel kuoana, walisali mara nyingi na kumwomba Bwana awaongoze.

Saints, 1:111–12

Ann na Newel wanapata ono.

Usiku mmoja wakati wa sala yao, Ann na Newel waliona ono. Katika ono, wingu lilitua juu ya nyumba yao. Walijawa na Roho wa Mungu. Wingu liliwazunguka. Kisha wakasikia sauti kutoka mbinguni. Ikawaambia, “Jitayarishe kupokea neno la Bwana, kwani linakuja.”

Saints, 1:111

Ann akijifunza kuhusu injili kutoka kwa Parley Pratt.

Baada ya muda, Parley Pratt alikuja Kirtland. Yeye na wenzake walifundisha injili ya Yesu Kristo. Mara tu Ann aliposikia kile walichofundisha, alijua kilikuwa cha kweli. Alienda nyumbani kushiriki habari hizo na Newel. Punde wakabatizwa.

Saints, 1:112

Joseph na Emma Smith wanakutana na Ann na Newel.

Miezi miwili baadaye, mwanamume na mwanamke walikuja kwenye duka la Newel. Newel hakuwajua, lakini mtu huyo alitikisa mkono wa Newel na kumwita Newel kwa jina lake. Mtu yule alisema, “Mimi ni Joseph nabii.” Alielezea kwamba Bwana alikuwa akijibu sala za Newel. Alikuwa amewatuma Emma na Joseph kukutana na Ann na Newel.

Saints, 1:113

Ann na Newel wanawaalika Joseph na Emma Smith kukaa nao.

Newel na Ann walijua maono yao yalikuwa yamekuwa kweli. Waliwaomba Joseph na Emma wakae nyumbani mwao. Ann na Newel walimpenda Yesu na injili Yake. Walitoa yote waliyokuwa nayo kwa Watakatifu na kwa Kanisa la Mwokozi.

Mafundisho na Maagano 38:23–27, 34–42; Saints, 1:114