“Hekalu la Kirtland Linawekwa Wakfu,” Hadithi za Mafundisho na Maagano (2024)
“Hekalu la Kirtland Linawekwa Wakfu,” Hadithi za Mafundisho na Maagano
Machi 1836
Hekalu la Kirtland Linawekwa Wakfu
Kuhisi Roho wa Bwana katika nyumba Yake
Baada ya takribani miaka mitatu ya kazi ngumu, Hekalu la Kirtland hatimaye lilikamalizika. Nabii Joseph aliwaalika Watakatifu kwenye mkutano maalum wa kuweka wakfu hekalu. Angesema sala maalum na kutoa hekalu hili kwa Bwana. Ingekuwa nyumba takatifu ya Bwana.
Saints, 1:235
Mapema asubuhi ya mkutano, mamia ya Watakatifu walijazana hekaluni. Wakati viti vyote vilipojaza, watu walisimama mlangoni na nje, wakiangalia kupitia madirisha. Kila mtu alifurahia kuona hekalu likiwekwa wakfu.
Saints, 1:235–36
Joseph alisoma sala ya kuweka wakfu hekalu. Alimwambia Bwana kwamba Watakatifu walikuwa wamemtii Yeye. Alimwomba Bwana akubali hekalu hili kama nyumba Yake.
Joseph aliomba kwamba kila mtu aliyekuja hekaluni ahisi nguvu za Bwana na kujua kuwa ni nyumba Yake.
Joseph pia aliomba kwamba endapo Watakatifu wakitenda dhambi, waweze kutubu mara moja. Alimwomba Bwana awape nguvu ya kushiriki injili Yake ulimwenguni kote. Baada ya sala, kwaya iliimba wimbo mpya unaoitwa “Roho wa Mungu.” Watu walijawa na shangwe. Walisimama na kumshukuru Bwana.
Mafundisho na Maagano 109:21–32; Nyimbo za Dini, na. 2; Saints, 1:237
Watu wengi waliwaona malaika hekaluni siku hiyo. Waliona mwanga mkali ukishuka kutoka mbinguni juu ya hekalu. Baadhi ya watu walisema ilionekana kama wingu; wengine walisema ilionekana kama moto. Wote walihisi kwamba hekalu lilikuwa mahali patakatifu. Kwa kweli sasa ilikuwa nyumba ya Bwana.
Saints, 1:237