“Kuondoka Nauvoo na Kwenda Magharibi,” Hadithi za Mafundisho na Maagano (2024)
“Kuondoka Nauvoo na Kwenda Magharibi,” Hadithi za Mafundisho na Maagano
Juni 1844–Julai 1847
Kuondoka Nauvoo na Kwenda Magharibi
Watakatifu wanafanya na kutimiza ahadi zao kwa Bwana
Joseph Smith alikuwa amefariki. Sasa Brigham Young na Mitume wengine waliliongoza Kanisa. Brigham alijua kwamba Watakatifu hawakuwa salama tena na Nauvoo. Ingewabidi kuondoka. Lakini kwanza, Bwana aliwataka wamalizie kujenga hekalu. Aliwataka kufanya maagano na Yeye na kuunganishwa kama familia.
Saints, 1:571, 579–80
Baada ya miezi michache, hekalu lilikuwa tayari kwa ajili ya watu kufanya maagano humo. Maelfu ya Watakatifu walikuja hekaluni. Brigham alikaa hekaluni hadi usiku wa manane ili kuwasaidia kufanya maagano na Bwana. Hatimaye, Brigham alimwambia kila mtu kwamba walihitaji kuondoka Nauvoo.
Saints, 1:582
Wakati Brigham alipoamka asubuhi iliyofuata, Watakatifu zaidi walikuwa wakisubiri hekaluni. Brigham aliwaambia hapakuwa na usalama kuendelea kukaa Nauvoo. Walihitaji kutafuta makazi mapya huko Magharibi. Aliahidi kwamba wangeweza kujenga hekalu jipya wakati watakapofika huko.
Saints, 1:582–83; 2:13–14
Lakini Watakatifu hawakuondoka. Walitaka kufanya maagano na Bwana kabla ya kuanza safari yao kwenda kwenye makazi mapya.
Saints, 1:583
Brigham aliona nyuso zao na kubadilisha mawazo yake. Alitumia siku nzima na siku inayofuata akiwasaidia Watakatifu kufanya maagano hekaluni.
Saints, 1:583
Sasa kwamba Watakatifu walikuwa wamefanya maagano na Bwana, ilikuwa ni wakati wa kuondoka Nauvoo. Brigham alijua Bwana alikuwa na mahali palipoandaliwa kwa ajili yao. Alikuwa amepaona mahali hapo katika ono. Walianza safari yao. Hali ya hewa ilikuwa baridi, na ardhi ilikuwa matope. Watu waliugua. Walikuwa tayari wanaishiwa na chakula.
Saints, 2:16–18, 20–21
Watakatifu walikuwa na umbali mrefu wa kwenda. Brigham alijiuliza ni kwa jinsi gani wangeweza kufanya safari ndefu na ngumu kama hiyo. Alisali kwa ajili ya msaada wa Mungu.
Saints, 2:46
Bwana alimpa Brigham ufunuo. Yeye alimfundisha Brigham jinsi ya kuwaongoza Watakatifu. Yeye alisema wanapaswa kusaidiana kuwatunza maskini.
Bwana alisema Watakatifu wanapaswa kukumbuka maagano waliyofanya naye. Kama wangefanya hivyo, Yeye angewabariki na kuwasaidia katika safari yao.
Mafundisho na Maagano 136:4, 11, 42; Saints, 2:47
Safari ilikuwa bado ngumu sana. Baadhi ya watu walifariki. Lakini kwa sababu ya maagano yao ya hekaluni, Watakatifu walijua wangewaona wanafamilia wao tena.
Miezi michache baadaye, Watakatifu wa kwanza waliwasili katika Bonde la Salt Lake mwaka 1847. Brigham Young alipoliona bonde, alisema, “Hapa ndipo mahali sahihi.” Ilikuwa mahali sawa sawa na pale alipokuwa ameona katika ono. Hapa ndipo Watakatifu wangekuwa salama. Hapa wangeweza kumwabudu Bwana na kufanya kazi Yake kwa amani.
Saints, 2:17, 64–67
Kwa miaka mingi, Watakatifu zaidi na zaidi waliwasili. Walijenga mahekalu mengi zaidi, mahali ambapo watu wangeweza kufanya maagano na Bwana. Waliwatuma wamisionari ulimwenguni kote kufundisha injili ya Yesu Kristo. Kanisa la Mwokozi liliendelea kukua, kubariki watoto wa Baba wa Mbinguni kila mahali.